Ilikuwa ndoto yangu kufunga harusi siku ya 'birthday' yangu - Akothee

Akothee alisisitza kwamba harusi yake yenye hadhi ya nyota tano itafanyika siku hii akisherehekea pia kuzaliwa kwake.

Muhtasari

• Msanii huyo alidokeza kuwa anasherehekea siku ya kuzaliwa kufikisha miaka 40 na ushee.

• Mama huyo wa watoto 5 anatarajiwa kufanya harusi yake ya pili, licha ya kuwa na wanaume tofauti zaidi ya watatu.

Akothee asherehekea siku yake ya kuzaliwa siku ya harusi yake
Akothee asherehekea siku yake ya kuzaliwa siku ya harusi yake
Image: Instagram

Msanii na mjasiriamali namba moja nchini Kenya, Esther Akoth almaarufu Akothee anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, miaka 40 na ushee.

Msanii huyo ambaye kwa Zaidi ya mwezi mmoja amekuwa akiwaaminisha mashabiki wake kuwa Jumatatu ya Aprili 10 ndio siku yake kubwa ya kufunga harusi ya kisasa na mpenzi wake mzungu aliyembatiza jina Mr Omosh, hata hivyo hajafanya hivyo na badala yake ameisherehekea siku hii kama yake ya kuzaliwa.

Hata hivyo, Akothee ambaye alionekana akishuka ndege na shela la harusi la bei ghali aliloagiza kutoka nje ya nchi, alisisitiza kuwa harusi yake ipo ila hakutaja itafanyika muda upi.

“Heri ya siku ya kuzaliwa Malkia Mama. Mama Taifa na MKE. Nisaidie Kumtakia ESTHER AKOTH KOKEYO HERI ya siku ya kuzaliwa ya Ghorofa ya 4 🎂 TAMAA YANGU kuu ilikuwa kuolewa katika siku yangu ya kuzaliwa. Happy Birthday mama, nakupenda AKOTH wangu,” Akothee alijiandikia ujumbe.

Baadi ya mashabiki wake mitandaoni wamekuwa wakisema msanii huyo huenda ni kiki tu anafukuzia na hakuna harusi itafanyika licha yake kusisitiza kwamba Aprili 10 itakuwa siku kubwa ya kusimamisha jiji.

Ikiwa itafanyika, hii ndio itakuwa harusi yake ya pili, baada ya ile ya kwanza aliyofanya akiwa mtoto mdogo na mume wa kwanza, harusi ambayo ilikuwa ya hadhi duni kulingana na yeye.

Msanii huyo alisema safari hii harusi yake itakuwa kinyume cha ile ya kwanza kwani itakuwa ya kuwatoa mahasidi macho pima, akiwa na shela la thamani la laki 7 kutoka ughaibuni.

Akothee alidokeza kuwa huenda dadake, Cebby Koks akahudhuria harusi hiyo, licha ya uwepo wa tofauti za kifamilia baina yao kwa muda mrefu.

Itakumbukwa mwezi Desemba mwaka jana wakati Koks alifunga harusi ya kitamaduni na mume wake, wakili Steve Ogolla, Akothee hakuhudhuria wala hakumuandikia ujumbe wowote wa kumhongera kwa kupata ndoa na harusi juu.