Elizabeth Lulu Michael: Nataka kupima UKIMWI 'live' na Mange Kimambi

Michael alitaka vipimo hivyo kufanya baada ya Mange kuandika stori kuhusu hali ya UKIMWI ya mwigizaji huyo.

Muhtasari

• Lulu alidokeza kuwa Kimambi aliandika stori iliyolenga kumchafulia jina kuhusu hali yake ya HIV.

• Kimambi ana mazoea ya kuvujisha video chafu za watu maarufu kwenye App yake akilenga kupiga hela kwa wale wenye uhitaji wa kutazama.

Lulu ataka kupima ukimwi na Mange Kimambi Live
Lulu ataka kupima ukimwi na Mange Kimambi Live
Image: Instagram

Mwigizaji kutoka Tanzania Elizabeth Michael almaarufu Lulu amemwandikia mwanaharakati wa mitandao ya kijamii Mange Kimambi ujumbe akimtaka wakaongozane kupima hali zao za virusi vya UKIMWI.

Michael katika ujumbe huo alidokeza kwamba Kimambi kuna hadithi aliyoifanya kuhusu hali ya ya UKIMWI ya Michael, jambo ambao lilionekana kuwa la kumsingizia.

Sasa kufuatia hilo, Michael alimjulisha Kimambi kama yuko tayari wakaongozane na kufanyiwa vipimo wote ‘live’ ili kubaini mbivu na mbichi.

“Dada Mange shikamoo, najua utashtuka sana na huu ujumbe ila kusema za ukweli mimi sina baya. Sasa kuna stori umeandika leo kuhusu virusi vyangu vya UKIMWI na mimi naona kama ni fursa ya hela…” Elizabeth Michael alianza.

Alitoa wazo lake kwamba katika fursa hiyo ya hela, wote ni wakutane halafu waongozane hadi kituo cha afya au kununua vifaa vya kupima virusi na kufanya vipimo hivyo wakiwa peke yao kinyemela.

Halafu matokeo yao Mange Kimambi ayaoakie kwenye App yake na kuwalipisha wale ambao watahitaji kuingia ili kuyaona, na hiyo itakuwa fursa nzuri ya kupata pesa ambazo mwisho wa siku watazigawana pasu kwa pasu.

“Sasa tufanye kupima live, mimi na wewe lakini, halafu tutafute namna kama utadumbukiza kwenye App au wapi ila watu walipie kuona kupima mpaka majibu. Halafu tugawane faida. Au unaonaje hapo dada? Mimi niko tayari sina baya,” Michael alisema.

Hata hivyo Michael alisema kuwa Mange siku zote si mtu wa kuaminiwa katika masuala ya hela kwa hiyo ni sharti watafute namna kisheria ili wasije wakapapurana baada ya miamala kufanyika.

Kwa kujibu ombi hilo, Mange alisema kuwa suaa la kupima 'live' halitatendeka kwani siku hizi wenye virusi wanatumia dawa za kupngua makali kwa hiyo haviwezi onekana.

Pia alisema kuwa habari kuhusu hali ya Ukimwi ya Lulu hakuingelelea yeye bali ilitoka gerezani, akijitetea kwamba hawezi kamwe kuzungumzia afya ya mtu wakati hajampima.

"Ila ujue nini? Mbona hata sio mimi niliesema hiyo habari? Habari imetoka gerezani sio kwangu. Mimi kama mimi siwezi ongelea afya ya mtu na huku sijampima."

Kimambi amejulikana sana kwa kuvujisha video za ukakasi za mastaa wa Tanzania ambapo anaipakia kwenye App yake na mtu kuiona ni sharti alipie kwanza.

Baadhi wanahisi msanii huyo anawalipa watu kurekodi video za wapenzi wao wakiwa uchi chumbani na baadae kumtumia ili kuzivujisha, jambo ambalo limejulikana sana nchini mwao kama ‘connection ya Mange’.

Koneksheni ya hivi punde na ambayo ilichafua hali ya hewa ni uvujaji wa video za utupu wa mwigizaji Irene Uwoya.