Irene Uwoya: Haya maisha sasa ni shida, leo nimekuta mgeni anaongeza maji ya ugali

“Na wewe ungepunguza moto,” Shabiki wake kwa jina Emmanuel Ringo alimjibu.

Muhtasari

• "Tunacho wageni haswa wale manotutembelea kutoka mikoani kuja mjini, ukiongeza maji ongeza na unga kwakweli", mwingine alisema.

Irene Uwoya atania kuwa alimpata mgeni wake akiongeza maji
Irene Uwoya atania kuwa alimpata mgeni wake akiongeza maji
Image: Facebook

Mwanamitindo na mwigizaji mkongwe Irene Uwoya amewachekesha mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuzua utani kuwa alimkuta mtu aliyekuwa mgeni wake ndani ya nyumba yake akiongeza maji ya ugali mekoni.

Kupitia Instagam yake, Uwoya alisema kuwa maisha yamekuwa magumu kila upande mpaka wageni sasa hawana heshima kabisa wakiwa katika nyumba za wenyeji wao.

“Haya maisha sasa ni shida, leo nimekuta mgeni wangu akiongeza maji ya ugali,” Uwoya alitania.

Haijulikani kama ni kweli ama ni utani tu alikuwa anazua kutokana na meme hiyo ambayo imekuwa ikizungumziwa mitandaoni kulinganisha baadhi ya mambo ya aibu ambayo mgeni anaweza kutwa akifanya kati ya kufumaniwa akiongeza maji ya ugali ili kiwango cha ugali kiwe kingi au kufumaniwa akijipima nguo na viatu vya mwenyeji wake.

“Na wewe ungepunguza moto,” Shabiki wake kwa jina Emmanuel Ringo alimjibu.

Tunacho wageni haswa wale manotutembelea kutoka mikoani kuja mjini, ukiongeza maji ongeza na unga kwakweli,” mwingine alizidisha utani.

Uwoya amekuwa mkimya kwa muda baada ya skendo ya kuvujishwa kwa picha na video zake za utupu kumchafua kwenye mitandao ya kijamii.

Ilisemekana kwamba video hizo zilivujishwa na mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi.