Kimambi azidi kuwateketeza, avujisha video chafu ya Irene Uwoya

Mange Kimambi ni mwanaharakati wa kimitandao mwenye hulka ya kuvujisha video chafu za watu mashuhuri

Muhtasari

• Wiki chache zilizopita, Kimambi alivujisha video chafu ya msanii Lulu Diva, suala lililomuathiri sana msanii huyo mpaka kulazwa.

Mwanasosholaiti na muigizaji Irene Uwoya
Mwanasosholaiti na muigizaji Irene Uwoya
Image: Instagram//IreneUwoya

Mwanasosholaiti na mjasiriamali Irene Uwoya ndiye mwathirika wa hivi karibuni wa Connection za mwanaharakati Mange Kimambi kumuanika hadharani mbele ya macho ya wanamitandao.

Uwoya ameingia kwenye chati za Kimambi baada ya mwanaharakati huyo kuipakia video chafu ya Uwoya akiwa uchi wa mnyama huku akionekana hajielewi kabisa kutokana na kile wengi wanasema ni ulevi ulifanya akalegema mpaka kuvuliwa nguo na video ya utupu wake kurekodiwa.

Mange Kimambi alipakia video hiyo kwenye App yake kama kawaida na kuwataarifu watu kuwa hatimaye amepata mwathiriwa mwingine mwenye alicheza katika anga zake na kumwanika.

Video hiyo imesambazwa pakubwa mitandaoni huku hadi Uwoya mwenyewe akionekana kujutia tukio lile na kusingizia ulevi kuwa chanzo cha kupatikana na Kimambi.

“Hamna kitu sipendi kama mtu anambie utaona …nitaona nini ambacho sijawahi ona MUNGU kaniumba na macho mawili yanaona vizuri sanaaa …wewe Nani? Nakwambia ushindwe kwa jina la YESU …ujumbe umefika na nimekujibu sina jipya la kuona,” Uwoya alionekana kumkemea Kimambi baada ya kumwanika bila huruma kama mtungo wa kambare wanaosubiri kukauka kabla ya kupakiwa.

Watu mbalimbali wametolea maoni kuvujishwa kwa video hiyo huku baadhi wakimlaumu Kimambi kwa kuvujisha video chafu za watu bila kujali jinsi hali hiyo itawaathiri katika jamii na katika maisha yao kwani wengi wao huwa ni watu mashuhuri ambao wanategemea mitandao na ushabiki kupata riziki.

Wengine waliwalaumu wasanii hao ambao ndio walengwa haswa wa Kimambi kwani hana haja ya kuvujisha video za mtu asiyejulikana hata akapewa bure. Kimambi tabia yake ni kuvujisha video za watu mashuhuri ili kuwavurugua na wengi walitupia kovu wasanii kwa kujitakia misiba mingine kama huo wa Uwoya kulewa na kujiachia tupu mbele ya Kamera.

Wiki mbili zilizopita, Kimambi alivujisha video ya utupu ya mwanamuziki Lulu Diva, tukio lililosemekana kumuathiri pakubwa Diva na mpaka kumpelekea kulazwa wengine wakisema alitaka kujiua.

Ikumbukwe wiki chache zilizopita Uwoya alikuwa mgeni mashuhuri katika hafla ya kanisa moja mjini Morogoro lililokuwa likiadhimisha miaka minane tangu kuanza kutoa huduma huku pia akiwa mgeni mashuhuri katika kuzungumzia kikundi cha kina mama kanisani hapo. Wengi baada ya kuona hivyo walikisia kwamba Uwoya mwisho wa siku ameupokea wokovu na kuacha mambo ya kihovyo ila ndio tena sasa limempata baya zaidi la kuchafua jina lake kabisa.

Sasa iko wapi faida ya kumpikia mgeni na mwenyeji kulala njaa?