Lulu Diva adaiwa kulazwa Hospitali baada ya video yake chafu kuenezwa mitandaoni

Baada ya video yake chafu kuvuja na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Muhtasari

•Waandishi wa Gazeti la IJUMAA walifika nyumbani kwake maeneo ya Mbezi[1] Beach jijini Dar na kupata hayupo pale, lakini kwa mujibu wa majirani, wakasikia kuwa amelazwa hospitalini.

•Wiki jana mitandao nchini Tanzania ilitokota kweli kweli wakati ambapo video chafu ya msanii na mjasiriamali Lulu Diva ilivujishwa.

Lulu Diva
Lulu Diva
Image: sreengrab

Msanii wa Bongo Lulu Abbas almaarufu Lulu Diva anadaiwa kulazwa hospitalini kutokana na mshtuko uliofuatia baada ya video yake chafu kuvujishwa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mnamo Alhamisi, waandishi wa Gazeti la IJUMAA walifika nyumbani kwake maeneo ya Mbezi[1] Beach jijini Dar na kupata hayupo pale, lakini kwa mujibu wa majirani, wakasikia kuwa amelazwa hospitalini.

 

 

Wiki jana mitandao nchini Tanzania ilitokota kweli kweli wakati ambapo video chafu ya msanii na mjasiriamali Lulu Diva ilivujishwa.

Katika video ambayo ilisambazwa pakubwa kwenye makundao mbali mbali ya kijamii,  mwanamuziki huyo ambaye pia anajiongeza kama muigizaji akifanya matendo ya mapenzi huku akiwa anajirekodi mwenyewe.

Video hiyo ilivujishwa na mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi kupitia App yake na hapo ndipo uhondo mzima ulianza kusambaa kote mitandaoni na Lulu Diva kugeuka kioja cha jamii.

Baadhi ya watu walijitokeza na kutoa maoni yao kuhusu kuvujishwa kwa video hiyo ya ngono ya Lulu Diva ambapo wamekikemea kitendo hicho huku wengine wakimkashfu Kimambi kwa kuvujisha mambo binafsi ya watu.

Lakini bado swali kubwa linabaki kujua mwenye alimfikishia Kimambi hiyo video kabla ya kuivujisha na kumdhalilisha mwanamke mwenzake kwa kuanika upuuzi wake mbele ya dunia nzima.

Ni sawa kabisa kwamba Lulu Diva Kafanya Ujinga lakini hakufanya vile ili watanzania waone sasa kwanini Mange Ampost? Hivi amekosa cha kupost mpaka aamue kumuanika Lulu mbele ya Dunia nzima?” aliandika kwa chukizo kubwa mtumizi mmoja kwenye mtandao wa Instagram.

Kulingana na wengi, Kimambi hakufaa kabisa kumuanika Diva kwa upumbavu wake, haswa ikizingatiwa kwamba ni mwanamke mwenzake.

Mdau huyo aliwataka watu waache kukishabikia kitendo cha Kimambi kumwanika mwanamke mwenzake na kusema kitendo kama hicho kinamkosesha Diva ujasiri hata wa kuonekana hadharani.

“Hautaamini siku ukimuona Ndugu yako wa Karibu akipostiwa Yupo Uch'' nadhani hapo ndipo utakuwa mwisho wa Kushabikia Ujinga. Endelea kuinjoy Connection za Wengine, siku ya kikukuta na wewe utajuta kuzaliwa,” mtumizi mmoja wa Instagram alisikitika.