"Tahidi High walinilazimisha kuvaa sketi, sikuwa huru na nafsi yangu," - Makena Njeri

Alikuwa akiyajibu maswali kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Muhtasari

• Njeri alisema sasa anapojitathmini nyuma anaona alifanya jambo la maana kujitambua na kuwa na ujasiri wa kusema.

Makena Njeri, Shoga
Makena Njeri, Shoga
Image: Instagram

Makena Njeri ambaye ni mtetezi wa haki za watu wa kushiriki mapenzi ya jinsia moja, LGBTQ+ amezungumzia maisha yake kipindi anaigiza katika kipindi cha runinga cha Tahidi High.

Akizungumzia suala hilo katika moja ya swali aliloulizwa na shabiki wake wakati wa Q&A kupitia Instagram yake Ijumaa, Makena alieleza  kinagaubaka jinsi alivyokuwa anahisi kulazimishwa kuvalia sketi katika kipindi hicho ambacho waigizaji walikuwa na uvaaji wa sare za shule rasmi.

“Ulikuwa unahisi aje kuvalia sketi katika kipindi cha Tahidi High, ni swali la ukichaa lakini nimekuwa nikitaka sana kujua hisia zako katika uvaaji ule,” mmoja aliuliza.

Makena alijibu kwa kusema kwamba swali kama hilo si la kuchekesha kwa sababu linamkumbusha enzi zile alipokuwa akiishi kama mtumwa kwa kulazimika kuvaa sketi hali ya kuwa Imani yake ilikuwa katika uvaaji wa muonekano wa kiume vile.

“Si jambo la kuchekesha hata kidogo. Kipindi kile nilikuwa nahangaika sana katika kujitambua kijinsia. Nina furaha kwamba hatimaye niliweza kujiongeza kwa ujasiri na kuishi kwa kusema ukweli wangu wa Imani yangu ya kijinsia,” Makena alijibu.

Pia mtangazaji huyo alisema kwamab wakati anapiga darubini za tathmini za maisha ya huko nyuma, anajiona kama ni mtu ambaye alikuwa anaishi utumwani kwa lengo la kuifurahisha jamii tu.

“Ninaangakia nyuma na najiona kama mtu ambaye alikuwa anajaribu kufurahisha jamii kwa kuisha maisha ya uongo,” aliongeza Makena.

Makena pia alisema kwamba mwanaume shoga mwenzake kwa jina Maina Levis amekuwa ndiye motisha wake mkubwa kwani yupo katika jamii kubadilisha mawazo finyu dhidi ya watu wenye mapenzi ya jinsia moja.

Mwanaharakati huyo alifichua jambo la kusikitisha kwamba watu wengi tu huku nje na ambao wako katika ndoa wamo katika mrengo huo wa mapenzi ya jinsia moja kisiri licha ya kuwa katika ndoa halali.