Makena Njeri: Ninataka kuwa na familia, muda ukifika nitabeba ujauzito

Mwanaharakati huyo wa LGBTQ alisema amekuwa akitamani kuwa na familia yake.

Muhtasari

• Makena alisema amekuwa akitaka kuwa na familia yake na muda ukifika bila shaka atalizingatia hilo la mimba.

Mwanaharakati wa LGBTQ, Makena Njeri
Mwanaharakati wa LGBTQ, Makena Njeri
Image: Instagram

Mwanaharakati wa kutetea haki za watu wenye Imani ya kuwa katika mapenzi na wapenzi wa jinsia moja, Makena Njeri hatimaye amezungumzia suala la iwapo atafika kiwango fulani katika maisha ambapo atahitaji mtoto na ni kwa jinsi gani atampata.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram akijibu maswali ya mashabiki wake moja kwa moja, Njeri aliulizwa kama kweli mtu mweney ukakamavu wa mwili kama wake wenye muonekano wa kiume almaarufu ‘Stud’ kwa lugha nyingine anaweza himili vishindo vya kubeba mimba.

“Wewe kaam mwanamke mwenye ukakamavu wa mwili unaokaa kiume zaidi unaweza stahimili kubeba mimba? Ikizingatiwa kwamba tayari ushatulia na mwanadada mwenzako na mnaanza familia pamoja kama mashoga,” Shabiki mmoja alimuuliza.

Makeba alishangaza wengi pale alipofunguka kwamba suala la yeye kubeba ujauzito wala si maamuzi magumu kwake na kusema kwamba kwa muda mrefu amekuwa akitaka mtoto ila muda wake haujafika, ukifika tu bila shaka atatafuta mtoto.

“Ndio! Kumbuka ninataka kuwa na familia. Kwa maana hiyo ni ndio, wakati mwafaka ukifika bila shaka nitakuwa tayari kabisa kustahimili hili,” alijibu njeri kwa mshangao wa wengi.

Njeri ambaye alikuwa muigizaji na pia mtangazaji wa kimataifa aliibuka miaka miwili iliyopita na kuweka wazi kwamba baada ya kuhangaika kujificha kwa muda mrefu, hatimaye amejiongeza kwa ujasiri na kutangazia umma Imani yake ya kingono kwamba yeye ni shoga.

Watu wengi waligawanyika katika makundi mawili huku wengi wakimzomea kwa kitendo hicho ambacho nchini Kenya kimesalia kuwa kinyume na sheria za ndoa, huku wengine wakimpongeza kwa kuiambia dunia ukweli wake kuliko kuficha na kuumia kwani mficha maradhi siku zote mauiti humuumbua.

Kweli wengi waliokuwa wakisema huenda anafukuzia kiki suala hilo waliamini pale ambapo mjasiriamali Michelle Ntalami alipoweka wazi kwamba wawili hao wamekuwa katika mahusiano ya kimapenzxi na kutangaza kwamab wameachana kwa sababu ya Njeri kuchepuka.