Watu watoa hisia zao baada ya video chafu ya mwanamuziki Lulu Diva kuvujishwa

Lulu Diva amewahi kuwa katika mahusiano na wqasanii wenzake Rich Mavoko na Lava Lava.

Muhtasari

• Watu walimkashfu Mange Kimambi kwa kumwanika mwanamke mwenzake katika uso wa dunia nzima kwa kuvujisha mambo yake ya ndani.

 

Msanii na muigizaji Lulu Diva
Msanii na muigizaji Lulu Diva
Image: Instagram

Nchini Tanzania mitadao imetokota kweli kweli usiku wa kuamukia leo ambapo video ya ngono ya msanii na mjasiriamali Lulu Diva imevujishwa.

Katik video ambayo imesambazwa pakubwa kwenye makundi mbali mbali ya mitandaoni, inamuonesha mwanamuziki huyo ambaye pia anajiongeza kama muigizaji akifanya kitendo cha ngono huku akiwa anajirekodi mwenyewe. Video hiyo ilivujishwa na mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi kupitia App yake na hapo ndipo uhondo mzima ulianza kusambaa kote mitandaoni na Lulu Diva kugeuka kioja cha jamii.

Baadhi ya watu wamejitokeza na kutoa maoni yao kuhusu kuvujishwa kwa video hiyo ya ngono ya Lulu Diva ambapo wamekikemea kitendo hicho huku wengine wakimkashfu Kimambi kwa kuvujisha mambo binafsi ya watu.

Lakini bado swali kubwa linabaki kujua mwenye alimfikishia Kimambi hiyo video kabla ya kuivujisha na kumdhalilisha mwanamke mwenzake kwa kuanika upuuzi wake mbele ya dunia nzima.

Ni sawa kabisa kwamba Lulu Diva Kafanya Ujinga lakini hakufanya vile ili watanzania waone sasa kwanini Mange Ampost? Hivi amekosa cha kupost mpaka aamue kumuanika Lulu mbele ya Dunia nzima?” aliandika kwa chukizo kubwa mtumizi mmoja kwenye mtandao wa Instagram.

Kulingana na wengi, Kimambi hakufaa kabisa kumuanika Diva kwa upumbavu wake, haswa ikizingatiwa kwamba ni mwanamke mwenzake.

Mdau huyo aliwataka watu waache kukishabikia kitendo cha Kimambi kumwanika mwanamke mwenzake na kusema kitendo kama hicho kinamkosesha Diva ujasiri hata wa kuonekana hadharani.

“Hautaamini siku ukimuona Ndugu yako wa Karibu akipostiwa Yupo Uch'' nadhani hapo ndipo utakuwa mwisho wa Kushabikia Ujinga. Endelea kuinjoy Connection za Wengine, siku ya kikukuta na wewe utajuta kuzaliwa,” mtumizi mmoja wa Instagram alisikitika.