Mwezi wa ndoa huu: Hatimaye Kamene Goro afunga harusi na DJ Bonez

DJ Bonez na Kamene wamekuwa wakichumbiana kwa zaidi ya miaka 5 na Kamene aliwahi kanusha kuwa chini ya shinikizo la kuolewa baada ya kufika miaka 30.

Muhtasari

• Kamene aliolewa hapo awali na hali mbaya aliyopitia huenda ilimwacha akiwa na kiwewe.

• Baada ya Akothee, Zari na Kasolo, Kamene ameingia kwenye orodha ya mastaa waliofunga ndoa Aprili.

Kamene Goro afunga harusi na DJ Bonez,
Kamene Goro afunga harusi na DJ Bonez,
Image: Instageam

Mtangazaji Kamene Goro na mpenzi wake wa muda mrefu DJ Bonez wamripotiwa kuvishana pete za ndoa katika sherehe ya faragha.

Mbunge wa Lang’ata ambaye ni rafiki wa karibu sana wa Kamene Goro alishiriki picha na video za tukio zima katika Instastories zake bila kusema kitu chochote.

Lakini kutokana na picha hizo, inaonekana kabisa ni shughuli ambayo wahusika wake wakuu walikuwa DJ Bonez na Kamene Goro, na ilikuwa siku yao ya kuvishana pete za harusi pasi na kutaka watu kujua.

Hafla hiyo inawaonesha watu wachache mno waliohudhuria huku meza ziliwa zimefunikwa kwa maanguli ghali na ya kipekee kwa watu wa karibu kwa wapenzi hao wawili.

Jalang’o alizungumzia tukuo hilo kwenye picha ambayo aliipakia dakika chache baadae, alisema kuwa ilikuwa ni ndoa haswa na wala si tukio la kuvishana pete za uchumba, akiwatakia kila la kheri.

“Mapenzi ni kitu kizuri na cha kufurahisha sana. Hongereni kwenu dada yangu Kamene Goro na mpenzi wako DJ Bonez katika siku ya harusi yenu. Nawapenda sana jamaa zangu,” Jalang’oo aliandika.

Vyanzo vya ndani vinadai kwamba wapenzi hao wawili wamekuwa wakichumbiana kwa Zaidi ya miaka mitano.

Kamene aliolewa hapo awali na hali mbaya aliyopitia huenda ilimwacha akiwa na kiwewe. Katika mahojiano ya awali alikanusha madai kwamba yuko chini ya shinikizo la kuolewa baada ya kugonga miaka 30.

Mwezi huu wa Aprili umekuwa wa Baraka na kismati ya ndoa kwa mastaa wengi kufunga harusi.

Msanii na mfanyibiashara Akothee alifunga harusi ya kifahari na mpenzi wake Mr Omosh huku pia Zari akiarifiwa kufunga harusi ya Nikkah na Shakib Cham.

Aidha, mwishoni mwa wiki jana pia msanii wa Akamba Stephen Kasolo alifunga harusi ya kifahari na mama wa binti yake.