Akothee ajivunia kufanya mitihani yake ya Shahada ya Biashara

Akothee alifanya mitihani yake katika chuo kikuu cha Mt Kenya.

Muhtasari

•Akothee aliwasihi waajiri wampe kazi Agosti atakapofuzu.

•Akothee alisema  kuwa ataelekea katika likizo yake ya baada ya harusi pindi tu atakapomaliza mitihani yake siku ya Jumamosi.

Akothee na mume wake Denis Shweizer
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Msanii Esther Akoth, almaarufu Akothee alijawa bashasha baada kufanya mtihani wa kozi yake ya biashara.

Siku ya Jumatano, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alidokeza kuwa ni siku yake ya tatu kufanya mitihani hiyo.  Akothee alisema kuwa katika siku tatu ambazo amekuwa akifanya mitihani, mume wake, Schweizer amekuwa akimpleka na kumsaidia.

Akothee pia alidai kuwa amekita kambi katika kozi  ya Rasilimali Watu (Human Resource). Alidokeza kuwa haijakuwa safari rahisi kwa kuwa  amekuwa akifanya kozi hiyo kwa miaka 14 sasa.

"Siku ya pili ya mitihani yangu ya mitihani yangu ya mwisho, waweza kuniandika kazi baada ya Agosti, imekuwa ni safari ya miaka 14 na nne shuleni, nitarudi pindi tu nitakapomaliza karatasi yangu ya mwisho Jumamosi saa kumi na mbili jioni. Tufanye wapi karamu?" alisema.

Akothee alisema pia kuwa akimaliza mtihani  ,wataenda kwenye likizo yao ya harusi ambapo anatazamia kupata ujauzito.

" Kisha niende likizoni nikapate ujauzito," alisema Akothee.

Baadhi ya wasanii kama vile Nameless na Wahu walimjibu.

" Hongera mama, nitakusaidia kutafuta kazi Agosti," alisema Wahu.

"Waah, mitihani tena," alishangaa Nameless.

Haya yanajiri siku chache baada ya Akothee kufunga ndoa na mume wake Denis Schweizer jina la matani Omosh katika hoteli ya kifahari ya Windsor, Nairobi. Harusi yake ilihudhuriwa na wanasiasa na watu maarufu nchini ikiwemo mke wa Raila Odinga, Winnie Odinga.

Harusi yake ilikuwa ya kifahari na yenye ufanisi mkubwa. Baada ya hapo , Akothee alitangaza kuwa atafanya harusi ya pili katika nchi ya Uswizi, anakotoka mume wake Omosh.  Alidokeza kuwa atawasafirisha wasimamizi wake wote nchini humo ambao walikuwa ni pamoja na Azziad Nasenya, Milly na Kabi wa Jesus, Janet Otieno, Jalang'o na mkewe kati ya wengineo.