Mambo yamechemka! Mamake CR7 avunja kimya mwanawe kuachana na mkewe Georgina

Bi Dolores Aveiro mwenye umri wa miaka 68 alinyoosha maelezo akikiteua kitendawili hicho ambapo alisema kwa kifupi kwamba "kila wanandoa hugombana".

Muhtasari

• Ripoti za vyombo vya habari vya Uhispania na Ureno mwezi uliopita zilidai kuwa mshambuliaji huyo 'amechoshwa' na mwanamitindo huyo wa Uhispania.

Ronaldo na mkewe kushoto na mamake kulia.
Ronaldo na mkewe kushoto na mamake kulia.
Image: Instagram

Baada ya wiki kadhaa za kuwepo kwa uvumi kuhusu uhusiano wa mchezaji Christiano Ronaldo na mkewe Georgina Rodriguez kuwa na mkwamo na kutishia kuvunjika, hatimaye mamake alinyoosha maelezo kuhusu hilo.

Bi Dolores amekanusha madai ya matatizo ya uhusiano kati ya nyota huyo wa soka na Georgina Rodriguez.

Ripoti za vyombo vya habari vya Uhispania na Ureno mwezi uliopita zilidai kuwa mshambuliaji huyo 'amechoshwa' na mwanamitindo huyo wa Uhispania na mshawishi na wanaweza kuwa katika hatihati ya kuachana.

Georgina, 29, alijibu kwa kukanusha ugomvi kati yake na mpenzi wake wa miaka saba, akiandika kwenye mtandao wa kijamii: 'Mwenye wivu huzua uvumi, mbezi hueneza na kipusa huamini.'

Siku kadhaa baadaye Cristiano, 38, alichapisha picha ya kimahaba kwenye Instagram yake ikimuonyesha akimbusu mwanadada huyo mrembo walipokuwa wakishiriki mlo na kinywaji na kuandika: 'Cheers to love.'

Dolores Aveiro, 68, alipuuzilia mbali pendekezo lolote kwamba uhusiano wa mwanasoka huyo na Georgina ulikuwa kwenye hali mbaya usiku kucha kwa kutaja madai hayo 'uongo' alipokuwa akihudhuria ufunguzi wa duka huko Madeira alikozaliwa.

Aliwaambia waandishi wa habari kuhusu tukio aliloalikwa katika mji mkuu wa kisiwa cha Funchal: 'Yote ni uongo. Kila wanandoa hubishana, lakini kilichoandikwa ni uwongo.'

Mama mzazi wa Cristiano tayari amemtembelea nyota huyo na familia yake katika mji mkuu wa Saudi Arabia Riyadh ambako ndiko makazi yao sasa.