Mwanamitindo Mitchell Ntalami aomboleza kifo cha mbwa wake

Ntalami alifichua kuwa chanzo cha kifo cha Pixel bado hakijafahamika.

Muhtasari

• Kulingana na taarifa kwenye Instagram yake alisema alimchukulia mbwa huyo kama mtoto wake na alimpenda sana.

• Mitchell alisema kuwa alimpa mbwa huyo jina la Pixel linayomaanisha rangi ndogo kwa kuwa alihisi alihitaji rangi ndogo maishani mwake.

Mitchell Ntalami na mbwa wake Pixel.
Mitchell Ntalami na mbwa wake Pixel.
Image: INSTAGRAM

Mjasiriamali na mwanzilishi wa Marini Naturals, Michelle Ntalami, anaomboleza kifo cha mbwa wake , Pixel.

Kulingana na taarifa kwenye Instagram yake alisema alimchukulia mbwa huyo kama mtoto wake na alimpenda sana.

Mitchell aliongeza kuwa mbwa huyo alimsaidia baada ya mahusiano yake kuvunjika na alielekeza mapenzi yake yote kwa mbwa huyo.

‘’Nilimpata wakati wa giza maishani mwangu. Nilikuwa nikipitia utengano na mchumba wangu, na nilihitaji kuelekeza mapenzi yangu kwa kitu ambacho ningehisi hakichukulii mapenzi yangu kwa uepesi.’’

Mitchell alisema kuwa alimpa mbwa huyo jina Pixel linalomaanisha 'rangi ndogo' kwa kuwa alihisi alihitaji rangi ndogo maishani mwake.

‘’Kwa kweli nilimpa jina la Pixel kwa sababu nilihitaji hilo tu; 'rangi ndogo' maishani mwangu," Ntalami aliongeza.

Kulingana na Ntalami mbwa huyo alimsaidia kukua kwa njia nyingi maishani kwake na kuwa alimfanya kujua kucheka na kupenda tena.

‘’Alinisaidia kukua kwa njia nyingi. Alinisaidia kucheka na kupenda tena. Nimtakosa sana’’

Ntalami alifichua kuwa chanzo cha kifo cha Pixel bado hakijafahamika, lakini anatumai ‘karma’ itamtendea haki.