"Tumetoka mbali" Mama Dangote aibua kumbukumbu na picha ya enzi za ufukara

“Maisha ni safari ndefu mwanangu Naseeb @diamondplatnumz 👫💙❤️..Tumevuka milima na mabonde Kwa uwezo wa M/mungu" - Mama Dangote.

Muhtasari

• Mashabiki wao waliona fahari katika tamko hilo la mama kwa mwanawe na kutoa maoni yao wakisema kuwa dua pekee ambayo ina ukweli ndani yake ni ile ya mama kwa mwanawe.

Diamond Platnumz akiwa na mamake enzi za ufukara.
Diamond Platnumz akiwa na mamake enzi za ufukara.
Image: diamond platnumz.

Picha ni sehemu nzuri sana ya kuhifadhi kumbukumbu za hatua ya safari yako kuelekea katika kesho yake yenye mwanga na tabasamu Zaidi kuliko jana na leo yako.

Mamake Diamond, Mama Dangote amewapa mashabiki wake kionjo cha kumbukumbu za zamani yake wakiwa bado ndio wanang’ang’ana kitoboa kimaisha na mwanawe Diamond.

Katika picha hiyo, Mama Dangote walionekana wakiwa na Diamond kwenye meza, msanii huyo akiwa ameshikilia mkononi kama tuzo za muziki ambazo alikuwa amejishindia kipindi anachipukia kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Flava.

Mama Dangote alitoa maelezo kiasi akisema kuwa imekuwa safari ndefu sana akimuona mwanawe Diamond aipiga hatua katika muziki mpasa sasa hivi anatambulika kama mfalme wa Bongo Flava katka ukanda wa Afrika Mashariki.

Mama Dangote alisema kuwa ni safari ambayo bila shaka yoyote imekuwa ikiongozwa na Mungu, na pia kuomba kuwa Mungu awalinde na mwanawe wanendelee kuishi na haswa yeye kuzidi kuyashuhudia mafanikio ya mwanawe.

Maisha ni safari ndefu mwanangu Naseeb @diamondplatnumz 👫💙❤️..Tumevuka milima na mabonde Kwa uwezo wa M/mungu bado anatushika mikono ..Tunaomba atufikishe mbele zaidi …Alhamdullillah 🤲” aliandika mama mtu.

Diamond ambaye siku zote ana ukaribu mkubwa na mama yake alimtupia makopakopa ya emoji za mapenzi mamake, akionesha shukrani ya siku zote kumpa shavu na himizo la kufanya muziki.

Mashabiki wao waliona fahari katika tamko hilo la mama kwa mwanawe na kutoa maoni yao wakisema kuwa dua pekee ambayo ina ukweli ndani yake ni ile ya mama kwa mwanawe.

“Dua pekee anayoomba mzazi kwa mtoto wake ni mafanikio mashaallah nasi allah atuongozee vizazi vyetu inshaallah,” mmoja alisema.

“Kila muomba mungu hachoki na akipata pia mungu ndo kila kitu,”

“Kwakweli Mungu ni mwema wasio elewa hua wanaona Kama mnalinga lakini ni wakati wa Mungu kuleni matunda “ Kudra Bihora alisema.