Rayvanny alikutumia akakuacha chunga na Mario pia- Fridah Kajala amshauri Paula

Kwenye video hiyo mama yake alikuwa akimwambia kuwa anatakiwa kuwa makini na mahusiano

Muhtasari
  • Mfano wa kisa kama hiki ni uhusiano kati ya Paula Kajala kijana maarufu wa Kitanzania anayejulikana kwa umaarufu wake kote Afrika Mashariki.
Kajala azungumzia bintiye kutaka kujiua na majuto ya siku za nyuma.
Kajala azungumzia bintiye kutaka kujiua na majuto ya siku za nyuma.
Image: Instagram

Fridah Kajala amezua gumzo mitandaoni baada ya video kuenea akimpa mwanawe Paula kuhusu mapenzi.

Mara kwa mara tumewaona watu mashuhuri wakiwa na uhusiano wa karibu na wanawe na hata kuwapa ushauri jinsi ya kuishi katika karne hii ya sasa.

Mfano wa kisa kama hiki ni uhusiano kati ya Paula Kajala kijana maarufu wa Kitanzania anayejulikana kwa umaarufu wake kote Afrika Mashariki.

Paula alipata umaarufu wake wakati yeye na Rayvanny walipokuwa wakichumbiana na kuonyesha mahaba yao kwa mashabiki wao.

Hata hivyo wapenzi hao walitengana mwaka mmoja uliopita na hawakufichua sababu ya kutengana. Baada ya kuachana , Rayvanny alirudiana na aliyekuwa mpenzi wake Fahyma kwani Paula pia alionekana kuendelea na Mario msanii wa bongo fleva kutoka Tanzania .

Hata hivyo leo video imeibuka kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Paula na mama yake Fridah wakizungumza huku mama yake akimshauri .

Kwenye video hiyo mama yake alikuwa akimwambia kuwa anatakiwa kuwa makini na mahusiano kwa sababu mwanzo Rayvanny alimtumia na kumtelekeza .

Alimwomba awe mwangalifu na Mario kwa sababu hajui nia yake.

"Rayvanny Amekutumia Kisha Amekuacha,Usikubali Na Marioo Akutumie Kisha Akuache,"Fridah alimwambia mwanawe.

Katika video iliyoenea mitandaoni mapema wiki hii Paula aisema kwamba ana imani kwa mpenzi wake Mario kumfanya mkewe.

"Wewe ni demu wa nani?" mwanamume ambaye alikuwa akimrekodi alisikika akimuuliza kwenye video hiyo.

Paula kwa madaha ya tausi alijibu, "Omary!"

Mwanamume huyo aliendelea kumuuliza mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 20 kama Marioo ana mpango wa kumuoa siku moja.

"Kwa nini isiwe hivyo?" Paula alijibu kwa sauti ya kijasiri.

Takriban wiki mbili zilizopita, Paula Kajala kwa hasira nyingi aliwasuta watu wanaoingilia maisha yake hasa ya mahusiano.

"Ifike mahala mheshimu maisha ya mtu binafsi, nina haki ya kuwa na mtu nimpendaye kama watoto zenu/ndugu zenu/na nyinyi wenyewe mnavyofanya (Tofauti yetu, nyinyi mnafanya gizani mimi ninawaonyesha)," alisema.