Alikiba avunja kimya baada ya kuonekana na 'bastola'

Mwishoni mwa wiki jana, Alikiba alionekana akiwa na kitu kilichodhaniwa kuwa bunduki kwenye kiuno chake akiwa amekiingiza kwenye suruali.

Muhtasari

• Alikiba alisema kuwa baadae alipoona maneno ya watu miqandaoni kuwa ilikuwa bunduki wala hakuhisi vibaya.

Alikiba aonekana na bastola, jinsi anavyojilinda
Alikiba aonekana na bastola, jinsi anavyojilinda
Image: Instagram

Siku chache baada ya msanii Alikiba kuonekana akiwa amejihami kwa kitu kilichodhaniwa kuwa bastola kwenye kiuno chake, msanii huyo amevunja kimya kuhusu tukio hilo.

Licha ya wengi kujiaminisha mia kwa mia kwamba ile ilikuwa bastola, msanii huyo amejitokeza wazi wazi na kukanusha madai hayo akisema kuwa kilichoonekana na kudhaniwa kuwa ni bunduki haikuwa bunduki kweli.

Kulingana na msanii huyo, kilichoonekana ni ‘speed light’ ya kamera ambayo ilikuwa inatumika katika upigaji picha kwa ajili ya kutambulisha jezi za timu yake ya Team Kiba ambayo itaenda kukutana na timu ya msanii matata Mbwana Samatta, Team Samatta.

“Hapana, haikuwa bastola. Watu unajua wanaweza wakaona chochote kile wakaongea wanachokijua. Lakini ukweli ilikuwa ni speedlight ya kamera. Sio bastola. Ile speedlight mpiga picha alinipa nikaichomeka hapa [akionesha kwa kiuno] bila kujua yaani,” alisema

Alikiba alisema kuwa baadae alipoona maneno ya watu miqandaoni kuwa ilikuwa bunduki wala hakuhisi vibaya.

“Unajua watu wanaweza kusema kitu chochote na huwezi kuwakataza,” alisema msanii huyo wa Mapenzi yanarun Dunia.

Wikendi baada ya watu kumuona na kitu hicho, walizua dhana mbali mbali ,baadhi wakijijazia kwamab ndio sababu kuu huwa hawamuoni akiwa amezingirwa na mabouncer wenye misuli iliyotuna kama wasanii wenzake wengine kina Diamond, Harmonize, Zuchu, Rayvanny na wengine.

Alikiba aonekana na bastola, jinsi anavyojilinda
Alikiba aonekana na bastola, jinsi anavyojilinda
Image: Instagram