Guardian Angel asema ndiye mwanamziki pekee wa injili anayeishi Karen

Mwanamziki huyo anamiliki biashara kathaa ikiwemo ya kufuga kuku.

Muhtasari

• Akizungumza na wanahabari wa runinga ya mtandaoni SPM BUZZ, alisema kuwa haungi mkono mapendekezo ya kuweka tozo ya 15% licha ya yeye kuwa na pesa nyingi.

• Guardian Angel alisema kuwa anapata hela za kutosha kutoka kwa muziki.

Image: Instagram

 Msanii wa wimbo za Injili Guardian Angel amefichua kuwa yeye ndiye msanii pekee wa nyimbo za Injili anayeishi mtaa wa kifahari wa Karen.

Mjasiriamali huyo alisema haya alipoulizwa kuhusiana na ushuru unaopendekezwa katika mswada wa fedha wa 2023 kwa  waunda maudhui ya kidigitali .

Msanii huyo alisema kwamba kamwe haungi mkono mapendekezo hayo licha ya yeye kuwa na pesa nyingi.

Maoni yake ya kupinga mswada huo unachochewa na wasanii na waunda maudhui wanaoteseka katika sekta ya muziki nchini Kenya.

“Mimi nina hela, mimi ndie msanii pekee wa injili anayeishi Karen. Ringtone anaishi Runda si Karen....na si ati apo si mahali unaeza kaa hivi hivi , naishi vizuri.” alisema Guardian Angel.

Aliongeza kuwa muziki wa Kenya unamlipa vizuri na anajimudu pakubwa kupitia muziki licha ya wasanii wengi nchini kusema kuwa muziki wa Kenya hauna pesa na haiwezi kumudu maisha yao.

“Ningekuwa nasema uongo mbele ya Mungu ambaye amenifungulia nikisema muziki hainilipi, muziki inanilipa poa, ndio maana nasema mimi muziki inanilipa sijasema inatulipa.”

Guardian mwenye umri wa miaka 34 aliibua gumzo mitandaoni mwaka jana baada ya kumuoa mke mwenye umri wa miaka 53.

Guardian Angel alijitosa kwenye ndoa na mama huyo wa watoto watatu mwezi Januari mwaka jana baada ya kuchumbiana kwa takriban miaka miwili. Wawili hao hata hivyo hawana mtoto pamoja.

Mwaka jana, mwanamuziki Guardian Angel aliweka wazi kuwa kupata watoto sio kipaumbele katika ndoa yake na Esther Musila.

Katika mahojiano ya Juni, mwanamuziki huyo wa nyimbo za injili alisema nguzo kuu ya uhusiano wao ni mapenzi na si watoto.

Guardian Angel alisema kwamba kupata mtoto na Bi Musila ni la ziada kutoka kwa Mungu  ambayo kwake si lazima wapate.

 "Nilipoingia kwenye ndoa yetu, mtoto ni nambari mbili. Akija ama akose ni sawa. Nambari moja ni upendo wetu. Mungu akitaka kutupatia bonasi ya baraka ya mtoto ni sawa. Lakini kama haipo, hiyo ni bonasi, tunafurahia na tulicho nacho. Upendo wetu ndio ninaojali," Guardian alisema katika mahojiano na Plug TV.

Mwanamuziki huyo alisema upendo wao pekee umetosha na kueleza kuwa umemletea amani kubwa moyoni.