YouTube: Chaneli ya Alikiba yadaiwa kudukuliwa, Elon Musk aonekana akiongea 'live'

Mwanamuziki huyo mwenye usiri mkubwa bado hajazungumzia suala hilo wala kutoa taarifa yoyote kutokana na madai hayo ya kudukuliwa.

Muhtasari

• Video za muziki wa msanii huyo zilikuwa zimeondolewa kwenye akaunti hiyo kwa takriban saa moja hivi na Mwanabiashara Elon Musk kuonekana akizungumza moja kwa moja

Image: Screengrab//CitizenTV

Chaneli ya Youtube ya mwimbaji maarufu wa nyimbo za Bongo, Alikiba imedaiwa kudakuliwa huku mmiliki wa mtandoa wa Twitter, Elon Musk akionekana akifanya video mubashara.

Video za muziki wa msanii huyo zilikuwa zimeondolewa kwenye akaunti hiyo kwa takriban saa moja hivi na Mwanabiashara Elon Musk kuonekana akizungumza moja kwa moja na watu zaidi ya milioni 8.1 wakimsikiza kwenye liv hiyo.

Video hizo aidha zimeonekana kurudishwa na akaunti yenyewe imerudishwa jina ya umiliki wa jina Alikiba baada ya jina ya akaunti hiyo kubadilishwa na kuitwa Teslla INC.

Mwanamziki huyo mwenye utata bado hajazungumzia swala hilo wala kutoa taarifa yoyote kutokana na madai hayo ya kudukuliwa.

Kampuni hiyo pia iliwai kudakua akaunti ya Diamond Platinumz miaka kadhaa iliyopita na ata msanii huyo alijitokeza na kualamikia swala hilo na kusema kuwa video za nyimbo yake imeondolewa.

Msanii huyo ambaye yupo nchini Kenya, ambapo anatarajiwa kutumbuiza katika jiji la Naivasha siku ya Ijumaa.

Kumekuwa na ongezeko wa kesi za akaunti ya Youtube na mitandao mengine kudukuliwa na watu asiofahamika huku wengine waiitisha hela ili kuweza kuridhisha umiliki wa akaunti hizo.