Jacque Maribe alikataa nifanye DNA - Eric Omondi

"Mimi sasa kuna venye nimekua nikitaka kufanya lakini ni kuna vile yeye hataki," alisema Eric.

Muhtasari

• Eric Omondi alifunguka kuwa ametaka kwa muda sasa kufanya DNA lakini amepokea vikwazo kutoka kwa mwanamke huyo.

Jackie Maribe na Eric Omondi walipopatana miezi michache iliyopita.
Jackie Maribe na Eric Omondi walipopatana miezi michache iliyopita.
Image: SIMON KABU

Mchekeshaji wa muda mrefu nchini Kenya, Eric Omondi amedai kuwa mwanahabari wa zamani wa Citizen Tv, Jackie Maribe amekuwa akimnyima nafasi ya kufanya DNA kwa mtoto anayedaiwa kuwa wake.

Mchekeshaji huyo ambaye sasa amegeuka kuwa mtetezi wa haki za wanyonge akizungumza na kituo kimoja cha radio cha humu nchini alifunguka kuwa ametaka kwa muda sasa kufanya DNA lakini amepokea vikwazo kutoka kwa mwanamke huyo.

“Umeipata bro, mimi sasa kuna venye nimekua nikitaka kufanya lakini ni kuna vile yeye hataki lakini sifai kuongelelea mingi kwa sababu kuna kesi mahakamani,” Eric alieleza baada ya mtangazaji huyo kumuuliza kama anazuiliwa kufanya DNA kwa mtoto huyo. 

Mapema mwezi huu, Eric Omondi alionekana kufurahia baada ya mpenzi wake Lynne kupata ujazito akisema kuwa mtoto huyo ndiye atakuwa mwanawe wa kwanza licha ya wanamitandao kufahamu kuwa ana mtoto na Mwanahabari huyo.

“Huyu atakuwa mtoto wangu wa kwanza kabisa, wa kwanza na Mungu amenibariki na wangu kabisaa. Sijui kama mtoto wangu na Jackie Maribe kama ni wangu lakini haina shida.”

Mnamo tarehe 8 mwezi Juni, mchekeshaji huyo ambaye amewai kushinda tuzo nyingi barani Afrika alitangaza kuwa hivi karibuni yeye na mpenzi wake watakuwa wazazi baada ya kupoteza ujauzito wao miezi saba iliyopita.

Mchekeshaji huyo mwenye umri wa miaka 41 akitangaza ujauzito huo alionekana kujilinganisha na Sarah kutoka katika Biblia ambaye alingoja kwa miaka mingi kabla ya kubarikiwa kupata mtoto wake mwenyewe.

“Imenichukua miaka 41 lakini hatimaye Mungu amenibariki na mtoto wangu Tunda la viuno vyangu! Najisikia kama Sara wa Ibrahimu wa Biblia, alingoja maisha yake yote kwa ajili ya mtoto wake mwenyewe,” ulisoma ujumbe huyo wa furaha.