Rosa Ree afunguka kuhusu "Una bwana na bwana ana bwana wake" kwenye wimbo mpya!

Hakutaka kuzungumza kama ni kweli baba mtoto wake anahusishwa na ushoga lakini alisema, "Kiufupi, ndio, na mimi naweza nikasema experience yangu imekuwa ni nzito lakini ndio."

Muhtasari

• Alisema kuwa mara nyingi yeye ukitaka kumjua anafikiria nini basi sikiliza muziki wake kwa sababu anayawasilisha mawazo yake mengi kupitia muziki..

• Msanii huyo alikataa kabisa kulizungumzia suala la baba mtoto wake.

Rosa Ree agusia mstari kuhusu ushoga kwenye wimbo wake mpya.
Rosa Ree agusia mstari kuhusu ushoga kwenye wimbo wake mpya.
Image: Screengrab//YuoTube

Rapa matata wa kike kutoka Tanzania, Rosa Ree baada ya kimya cha muda, amerejea na kazi mpya ambapo katika moja ya kazi hizo, anasikika akitema madini katika mstari ambao umedakiwa na watu wengi kuwa “Una bwana na bwana ana bwana wake”.

Wengi wamekuwa wakiutafsiri mstari huo kwa njia tofauti tofauti baadhi wakihisi kwamba alikuwa anampiga makombo aliyekuwa mpenzi wake ambaye ndiye anakisiwa kuzaa naye.

Lakini katika mahojiano na Refresh ya Wasafi, Rosa Ree amefunguka ukweli halisi wa mstari huo akisema kwamba kwenye maisha ya Sanaa haswa wasanii huimba vitu au mambo ambayo aghalabu hutokea, hata kama si kwao wenyewe lakini kwa watu wengine.

“Kwanza kwenye Sanaa tunaimba mambo mengi sana, lakini naangalia pia vitu halisi ambavyo vimetokea kwenye jamii, natumia uzoefu wa watu wengi. Kwa hiyo kuna vitu vingine naeza nikawa nimeviona hata kwa jirani nikawa nikasema, eh mtu Fulani alipitia kitu Fulani unajua, na ikaweza kumgusa mtu,” Rosa Ree alisema.

“Hata ile line au punchline nyingine kali ambazo ninazo zinakuwa zimewagusa watu kwa sababu na wao wanakuwa wamepitia kitu ambacho kiko kama hicho au kama sio hicho ni hicho hicho basi.”

Msanii huyo hata hivyo hakujibu moja kwa moja kama mstari huo ulikuwa unalenga kwa baba mtoto wake akisema;

“Kiufupi, ndio. Kwenye maisha lazima ukipitia maisha lazima upitie mambo mengi. Na ndio, na mimi naweza nikasema experience yangu imekuwa ni nzito lakini ndio maana tunakuwa tunasema, eeh, kumbe sisi ni wababe. Kumbe kweli maisha yanaweza yakakupiga hivi na wewe uweze kuyakabili vile, ni maisha,” Rosa Ree alielezea.

Alisema kuwa mara nyingi yeye ukitaka kumjua anafikiria nini basi sikiliza muziki wake kwa sababu anayawasilisha mawazo yake mengi kupitia muziki.

“Mimi ni kama kitabu kiko wazi kabisa, unaweza ukasoma ukajua Rosa Ree anafikiria nini, kitu gani anapitia, sasa hivi yuko katika hali gani, utajua tu kupitia muziki wangu,” alisema.