Alikiba? Kwa nini nisimpende, nampenda zaidi ya sana - Niffer

"Ni mtu ambaye hajawahi nifanya nifanye vitu vya kipuuzi, kwa hiyo kwa nini nisimpende? Nampenda kwa sababu ni mtu mzuri kwangu, na ni mtu mzuri pia kwa jamii,” - Niffer .

Muhtasari

• Yaani mtu akiwa mzuri, nguvu yake inakushawishi wewe kuwa na nguvu chanya pia - Niffer alisema.

• “Mara ya kwanza tunakutana na Ali ni 2009, tulikutana tu yaani kwa njia nzuri, tukaanza kufanya kazi,” alisema.

Niffer akiri mapenzi yake kwa Alikiba.
Niffer akiri mapenzi yake kwa Alikiba.
Image: Instagram

Niffer kwa mara ya kwanza amezungumza ni lini walianza kujuana na Alikiba na hata kuanza kumvisha katika matamasha maalum ambayo msanii huyo amekuwa akitumbuiza.

Kwenye mahojiano ya chaneli ya Ayo TV, Niffer alifunguka kwamba mara ya kwanza wamekutana na Alikiba ilikuwa mwaka 2009 na ilikuwa kwa njia nzuri tu kabla ya kufahamiana na kuanza kufanya biashara pamoja.

“Mara ya kwanza tunakutana na Ali ni 2009, tulikutana tu yaani kwa njia nzuri, tukaanza kufanya kazi,” alisema.

Mrembo huyo hata hivyo alisita na kupata kigugumizi kidogo alipoulizwa kama ikitokea Alikiba amemalizana kabisa na mke wake Amina Khalef, anaona kama anaweza kubali kuwa mke wa msanii huyo.

“Wewe unaonaje? Unaezataka iwe hivyo? Mimi sina lolote la kusema kwa hilo kwa sababu mwisho wa siku Allah ndiye anayepanga kila kitu. Japo sitamani kuolewa na msanii lakini si kigezo. Mimi namuomba Mungu na Mungu ndio anajua kaniandikia nani,” Niffer alificha jibu lake.

Lakini pia Niffer hakuweza kujizuia kukiri mapenzi yake kwa msanii huyo akisisitiza kwamba ni mtu mzuri na anahitaji mapenzi na maombi ya mafanikio kwenye kazi zake.

“Alikiba? Kwa nini nisimpende, nampenda sana na namheshimu sana na namtakia kila la kheri kwenye biashara zake, kwenye muziki wake… ni mtu mzuri. Yaani mtu akiwa mzuri, nguvu yake inakushawishi wewe kuwa na nguvu chanya pia. Ni mtu ambaye hajawahi nifanya nifanye vitu vya kipuuzi, kwa hiyo kwa nini nisimpende? Nampenda kwa sababu ni mtu mzuri kwangu, na ni mtu mzuri pia kwa jamii,” Niffer alitema ya moyoni.

“Alikiba ni mtu mzuri, yaani kwangu mimi ili kuwa mtu wangu katika maisha yangu, ni lazima uwe mtu mzuri kwanza,” aliongeza.