Sina mpango wa kutafuta mke tena, hata kienyeji sikupata! - Daddy Owen

Owen aianzisha kampeni ya kutafuta mrembo kienyeji wa kuziba pengo la mkewe aliyemtaliki mwaka jana lakini amedhibitisha hakufanikiwa kumpata.

Muhtasari

• Msanii huyo miezi saba iliyopita alitangaza kumtafuta mrembo wa kienyeji ambaye angeziba pengo la mkewe aliyemtaliki,

aeleza kwa nini hana haja ya kutafuta mke tena
Daddy Owen aeleza kwa nini hana haja ya kutafuta mke tena
Image: Facebook

Daddy Owen kwa mara nyingine amezungumzia kampeni ya kutafuta msichana wa kijijini maarufu Kienyeji mwishoni mwa mwaka jana.

Katika mahojiano ya kipekee kwa njia ya simu na mwandishi wa Radio Jambo, Owen alisema kuwa katika kampeni yake ya kujaribu bahati katika kupata mrembo wa kijijini wa kumuoa, hakufanikiwa licha ya kuchukua muda mrefu kutafuta mmoja.

Owen alisema kuwa hata hivyo, pia alishikika sana na kazi nyingi kiasi kwamba alipoteza azma ya kumpata mmoja.

“Mimi sikufanikiwa, kazi imekuwa nyingi. Sasa hivi, kazi imekuwa nyingi hata sina mpango wa kutafuta tena,” Daddy Owen alijibu.

Msanii huyo miezi saba iliyopita alitangaza kumtafuta mrembo wa kienyeji ambaye angeziba pengo la mkewe aliyemtaliki, huku akitaja baadhi ya sifa na vigezo – kigezo kikuu kikiwa ni msichana wa mashambani.

Warembo mbalimbali akiwemo mwanablogu wa YouTube Pritty Vishy walijitokeza kumtaka kuwachukua kama mkewe lakini Owen alidai kwamba wote waliojitokeza hawakukidhi vigezo vyote amabvyo alikuwa anavihitaji.

Kwa sasa baada ya kukosa kumpata msichana kienyeji, msanii huyo anajishughulisha na kituo cha kuwahudumia watoto wenye ulemavu kilichoko maeneo ya Kijabe kwa jina CARE.

Owen aliweka wazi kwamba kituo hicho tayari kimekamilika na kimeanza shughuli za kuwahudumia watoto, ikiwemo ni upanuzi mkubwa wenye vyumba mpaka vya watoto hao kukubaliwa kuja na kuishi pale na wazazi au walezi wao.