Ukizaliwa Kenya tayari una maarifa kama ya mtu wa form 6, ujuaji mwingi! - Pasta Mgogo

“Wakenya wanajifanya kama hawajui, kitu tatizo ujuaji mwingi. Shida ya Wakenya, yaani ukizaliwa Kenya tu, tayari, form 6! Ndio maana fujo nyingi mnazozifanya, sio kwamba hamjui mnachokifanya. Mnajua!"

Muhtasari

• “Unajua hawajui kwa nini bei ya unga Kenya ilipanda? Wanajua kwamba mahindi mlikuwa mnachukua Tanzania" - Mgogo alisema.

adai Wakenya wana ujuaji mwingi usiosaidia.
Pastor Mgogo: adai Wakenya wana ujuaji mwingi usiosaidia.
Image: Facebook

Mchungaji maarufu kutoka Tanzania, Daniel Mgogo amesema kwamba Wakenya wana ujuaji mwingi wa kujifanya kujua kila kitu ndio maana wanafanya fujo nyingi kila mahali kutoka mitandaoni hadi mitaani.

Katika klipu moja ambayo alipakia kwenye Facebook yake akihubiri wikendi iliyopita, Mchungaji Mgogo alisema kwamba Wakenya wanajitoa akili tu kujifanya hawajui kitu hali ya kuwa wanajua chanzo cha kila kitu kinachoendelea nchini, ikiwemo bei ya juu ya unga.

“Wakenya wanajifanya kama hawajui, kitu tatizo ujuaji mwingi. Shida ya Wakenya, yaani ukizaliwa Kenya tu, tayari [una maarifa kama mtu wa] form 6. Ndio maana fujo nyingi mnazozifanya, sio kwamba hamjui mnachokifanya. Mnajua mambo mengine ni hali halisi, yaani mnajitoa ufahamu tu,” Mchungaji Mgogo alisema.

Mchungaji huyo alisema kuwa Kenya ilikuwa inachukua mahindi kutoka Tanzania lakini wakati taifa hilo tegemezi lilipigwa na ukame, hali ilibadilika.

“Unajua hawajui kwa nini bei ya unga Kenya ilipanda? Wanajua kwamba mahindi mlikuwa mnachukua Tanzania, huku jua lilipiga mahindi hatukuvuna na sasa mahindi yaliyopatikana ni kwa bei. Kwa hiyo wakinunua na kusafirisha, ni lazima bei ya unga itapanda. Mnajua! Ila mnasumbua tu watu, mko barabarani ‘bei ya unga! Bei ya unga!’”

“Sio kwamba hawajui kwamba Kenya hakuna visima vya mafuta. Mafuta yanatoka nje, wanaopandisha bei ni wauzaji wale wa nje. Na hivyo lazima yapande bei, lakini utawasikia tu, heey mafuta yako juu…Akili nyingiiii…” Mchungaji huyo alisema.