Andrew Kibe kufanya DNA na babake ili kubaini iwapo kweli yeye ni mwanawe

"Ninafikiria sana kufanya DNA juu mimi na baba yangu hatuelewani," alieleza Andrew Kibe.

Muhtasari

• Mtangazaji huyo wa zamani wa redio alieleza kuwa amekuwa akitaka kujua iwapo mwanaume huyo ndiye babake mzazi na kuondoa mashaka yaliyojaa akilini mwake.

• Kulingana na Kibe, uamuzi wa kufanyiwa DNA ulitokana na uhusiano mmbaya kati yake na babake ambao umedumu kwa miongo kadhaa.

Muunda maudhui wa Marekani, Andrew Kibe.
Muunda maudhui wa Marekani, Andrew Kibe.
Image: INSTAGRAM

Mtayarishaji wa maudhui anayeishi Marekani, Andrew Kibe amefichua kuwa ana mpango wa kufanyiwa msumbujeni (DNA)  na babake ili kubaini iwapo kweli yeye ni mwanawe.

Akishiriki mipango yake na wafuasi wake kwenye mitandao yake ya kijamii, mtangazaji huyo wa zamani wa redio alieleza kuwa amekuwa akitaka kujua iwapo mwanaume huyo ndiye babake mzazi na kuondoa mashaka yaliyojaa akilini mwake.

"Ninafikiria sana kufanya DNA juu mimi na baba yangu hatuelewani na kumshtua mamangu, kama alikuwa na uhusiano nje ya ndoa, atalia. Ninapotua Kenya, jambo la kwanza nitakalofanya ni kupata DNA ya baba yangu na mimi,” alisema.

Mtangazaji huyo wa zamani wa radio  aliwafichulia mpango wake wa kupata chembechembe za DNA ya baba yake.

“Hivi ninavyomnunulia nyama choma na Guinness na nimuone akikohoa, nitampa kitamba na kumwambia akohoe hupo. Akimaliza nitamwambia anipe kitamba kicho niende nitupe. Nitakichukua na kupeleka maabara na kuwaambia hii ni ya baba yangu na niwaambie walinganishe na DNA yangu."

Kulingana na Kibe, uamuzi wa kufanyiwa DNA ulitokana na uhusiano mmbaya kati yake na babake ambao umedumu kwa miongo kadhaa.

“Bro, mimi na baba hatuelewani na kiukweli sijui kwanini huwa hatuelewani. Mbona hatuelewani buda? Mimi ndiye nongwe au wewe? Lazima tujue kwa sababu mmoja wetu ni nongwe,” alisema.

Mwanahabari huyo mwenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii, aliendelea kueleza kuwa iwapo atagundua babake si mzazi wake wa kumzaa ataelewa kwa nini wanazozana kila mara.

Hata hivyo matokeo hayo yalibainisha kuwa mwanaume huyo ni baba yake wa kweli, ataachwa bila chaguo ila kumkubali jinsi alivyo na labda kujaribu kuboresha uhusiano wao.