Mwanatiktok Nyako Pilot amuonya vikali Andrew Kibe baada ya kumuita 'Bootleg Akothee'

Drama imejitokeza kati ya Kibe na Nyako kutokana na maoni yake kuhusu matamshi ya TikTok.

Muhtasari

• Kibe kwenye chaneli yake mnamo siku ya Alhamisi, Mei 18 alimwita 'bootleg Akothee'.

• "Umebisha mlango mbaya vibaya hmmm," Nyako alimuonya Kibe.

Mwanatiktok wa Kenya Nyako Pilot amemsuta Andrew Kibe kwa kutoa maoni mabaya dhidi yake kwenye chaneli yake ya YouTube.

Kibe kwenye chaneli yake mnamo siku ya Alhamisi, Mei 18 alimwita 'bootleg Akothee'. "Yuko mtandaoni anapiga kelele, usipatie Mjaluo doh, hawatakuacha ulale."

Kibe alimkashifu kwa kujisifia kuwa nje ya nchi.

"Hakuna jambo la kuchukiza kama kuona mwanamke mzee akiongea upuuzi," Kibe alisema kwa maoni yake.

Nyako alimuonya Kibe na wakati huo huo akatishia kumchukulia hatua. Alisema Kibe hawezi kuwashambulia Wamarekani kwa sababu ya sheria zao kali za faragha, ikilinganishwa na Wakenya ambapo Kibe anachukua fursa ya mapungufu katika sheria za Kenya kuwanyanyasa wanawake.

"Ninajua jinsi Amerika inavyofanya kazi, nitaje tena na huo mdomo wako inanuka kwanza naenda Kenya. Ninaweza hata kwenda kwa ubalozi wa Marekani na kukuripoti," Nyako alimfokea Kibe kwenye kipindi cha moja kwa moja cha TikTok.

Aliongeza;

"Nifungulie mdomo wako ina nuka tena ati unatafuta views. Uta pata hizo views, utanipata Kenya. Unacheza na mfumo wa kimarekani, umeshinda umebully watu umebully watu nobody say nothing about that Andrew Kibe, maana Andrew Kibe ndiye mwenye kauli ya mwisho. kuhusu wanawake, acha Andrew Kibe," alizindua kwa lugha yake ya asili

"Umebisha mlango mbaya vibaya hmmm," alionya huku akimalizia.

Bifu hii imewasisimua Wakenya ambao wamefurahishwa na drama kati ya hao wawili.