'Mali yako ishaliwa' wanamitandao wamuambia Karen, Sue Gecambi akimmezea mate Samidoh

“Muangalie mwanaume huyu mtanashati, ana mwonekano mzuri, Kitafunio cha kukula mara moja." alisema Sue.

Muhtasari

• Sue Gecambi ammemezea mate mwanamuziki wa nyimbo za Mugithi, Samuel Muchoki  almaarufu Samidoh.

• Mwanzoni mwa mwezi huu, wawili hawa walirushiana vijembe mitandaoni chanzo, mwanaume Samidoh.

Sue Gecambi ammezea mate mpenzi wa seneta Karen Nyamu, Samidoh.
Sue Gecambi ammezea mate mpenzi wa seneta Karen Nyamu, Samidoh.

Mtayarishaji wa maudhui na mfanyibiashara anayeishi Marekani Sue Gecambi ammemezea mate mwanamuziki wa nyimbo za Mugithi, Samuel Muchoki  almaarufu Samidoh na kuibua gumzo mitandaoni wakimuonya senata Karen kuwa mpenzi wake yuko njiani kutengana naye.

Sue aliamka siku ya Jumatano akiwa ameangazia macho yake kwa mwanamuziki huyo anayezingirwa na utata kuhusiana na maisha yake ya mapenzi.

“Muangalie mwanaume huyu mtanashati, ana mwonekano mzuri, Kitafunio cha kukula mara moja. Boo” aliambatanisha ujumbe huo na emoji ya mapenzi.

Mwanzoni mwa mwezi huu, wawili hawa walirushiana vijembe mitandaoni chanzo, mwanaume Samidoh.  Vita hivyo viliibuka pindi tu Sue Gacambi alipoelekea katika akaunti yake ya TikTok na kutupa makombora kwenye kambi ya Karen.

Sue alidai kuwa licha ya mke wa Samidoh, Edday kumuachia mwanaume huyo bado  hajafunga ndoa naye.

“Wewe uliachiwa Samidoh, alikuachia akakuambia chukua Samidoh fanya kitu yoyote na yeye. Hajawai kuoa my dear. Atleast angekuoa wakati umeachiwa Samidoh Kenya na akaenda majuu.”

Kulingana na Sue, Samidoh hakuwa akimpenda Karen na alikuwa akimtumia tu kukata kiu chake.

“Hajawahi kuoa, samidoh hakupatii pete. Kazi tu ni kulala na wewe na tuko wengi tunataka kulala naye na tunampenda wengi bana.”

Seneta Maalum Karen Nyamu ambaye siku zote huonekana kuwa tayari kurusha masumbwi hakuchelewa kuingia uwanja wa vita na kumjibu mfanyibiashara huyo akisema kuwa matusi yake hayatazuia mpenzi wake Samidoh kumpokea katika uwanja wa ndege atakapo rejea kutoka safari yake nchini Uswizi.

Karen Nyamu akimjibu mfuasi wake mmoja aliyeonekana kumshabikia Sue katika akaunti yake ya Instagram, alilinganisha matusi ya Sue kama kelele za chura ambazo haziwezi mzuia Ng’ombe kunywa maji.

"Skia ujinga. Nini imebadilika baada yake kunitusi ama sasa Samidoh hatanichukua airport nikiland?” aliuliza Karen kwa kejeli kwa shabiki huyo."

Kiongozi huyo wa chama cha UDA, aliendeleza mashambulizi yake katika akaunti yake ya Facebook akisema kuwa hakutishwa na matusi yake na Sue achunge machungu yake kwake yasisababishe ajitoe uhai.

“Matusi tu? Bora nisiskie amejinyonga sababu ya machungu na maisha ya Karen Nyamu.”