Eric Omondi atua Uganda akiwa ameketi ndani ya kiatu, mavazi ya gunia - video

Katika video, Omondi alionekana ameketi kwenye upande wa usukani na kuendesha kiatu hicho katika barabara moja ya lami ambayo haikuwa na magari.

Muhtasari

• Alisema kuwa aliona hakuna haja ya kutembea ndani ya kiatu wakati kuna uwezo wa kuendesha kiatu hicho kama kigari kidogo.

Eric Omondi ndani ya kiatu
FASHENI Eric Omondi ndani ya kiatu
Image: Instagram

Mchekeshaji namba moja ukanda wa Afrika mashariki ambaye anajiita rais wa ucheshi Afrika, Eric Omondi kwa mara nyingine tena ameonesha ubunifu wake katika mavazi na mapambo yake ya kipekee.

Safari hii, Omondi ambaye alikuwa anelekea Uganda aliwashangaza wengi baada ya kuonekana barabarani akiwa ameketi ndani ya kigari kidogo kilichokuwa na muonekano wa kiatu ambapo pia ndiye alikuwa anakiendesha.

Omondi alisema kuwa ameshatua katika uwanja wa ndege na alikuwa anaelekea katika sehemu ya tukio akiwa anaendesha kiastu chake na aliposhuka alikuwa amepiga pamba ya gunia kutoka juu mpaka chini – muonekano wa fasheni ya kipekee ambaye Omondi pekee ndiye mtu wa kuiasisi.

Alisema kuwa aliona hakuna haja ya kutembea ndani ya kiatu wakati kuna uwezo wa kuendesha kiatu hicho kama kigari kidogo.

“UGANDAAA!!!!🇺🇬🇺🇬🇺🇬 Niko njiani kuelekea Uwanja wa Ndege. Kwa nini utembee kwenye VIATU huku unaweza Kuendesha gari ndani yake,” Omondi alisema.

Mchekeshaji huyo ambaye siku za hivi karibuni amekengeuka kuwa mwanaharakati wa haki za kibinadamu na mkosoaji mkuu wa utawala wa rais Ruto alikuwa miongoni mwa mamia ya watu waliohudhuria tamasha la Comedy Store lililofanyika katika uwanja wa ndege wa Kololo viungani mwa jiji la Kampala usiku wa Ijumaa.

Tamasha hilo lilikuwa linaongozwa na mchekeshaji maarufu Uganda Alex Muhangi na kando na vichekesho, liliwashuhudia wasanii mbali mbali wakitumbuiza akiwemo Nameless wa Kenya na kufunikwa kabisa na Diamond Platnumz kutoka Tanzania.