Mchekeshaji Eric Omondi asutwa baada ya kuibuka na mavazi ya ajabu

Eric alivalia nguo za karatasi nyeusi ambazo baadhi ya wanamitandao walizitaja kuwa takataka.

Muhtasari

•Baadhi ya wanamitandao walimkejeli na kumtania huku wakishangaa ni kwa nini aliamua kuvaa nguo kama hiyo.

•Wengine walimshauri dhidi ya hatu hiyo na kumweleza kuwa angehisi joto kwa kuvalia karatasi nyeusi wakati wa jua.

Eric Omondi

Mchekeshaji Eric Omondi amegeuka gumzo baada ya kupakia picha akiwa amevalia vazi la karatasi.

Omondi alipakia picha hizo Instagram na kutangaza kuwa anapanga safari kuenda Uganda leo Ijumaa usiku.Alikuwa amevalia nguo za karatasi nyeusi ambazo baadhi ya wanamitandao walizitaja kuwa takataka.

Baadhi ya wanamitandao walimkejeli na kumtania huku wakishangaa ni kwa nini aliamua kuvaa nguo kama hiyo.

"Hili ni nini umevaa?" mwanamitandao mmoja aliuliza.

"Kwa vazi hilo hutapita kwenye uwanja wa ndege Tanzania kwani haturuhusu makaratasi ya plastiki," mwingine alisema.

"Ndio maana sipati karatasi zangu za takataka, kumbe umezivaa," alisema mwingine.

Wengine walimshauri dhidi ya hatu hiyo na kumweleza kuwa angehisi joto kwa kuvalia karatasi nyeusi wakati wa jua.

Omondi amejulikana kuwa na njia nyingi za kuhakikisha jina lake linazidi kukolea na kusambaa miongoni mwa mashabiki. Hivi majuzi tu alikuwa ameibuka na mtindo wa nywele wa kushangaza.

Amejulikana pia kugiza kama mwanamke, Divalicious, huku akivalia nguo na viatu vya kike na hata kupodolewa.

Zaidi ya hayo, Waganda wengine walimkemea kuenda nchini mwao kama anavyowakemea wasanii wengine wakija nchini Kenya.

Baadhi walisema kuwa kuna uwezekano wa wao kumzuia kuhudhuria hafla yake nchini humo.