DJ Brownskin amkumbuka marehemu mkewe kwa ujumbe wa kuliza

"Siwezi tafakari uchungu ninaopitia na nitatoa kitu chochote ili kusikia kupumua kwako, najua bado unaishi maisha yako hata baada ya kufa…nitakumiss sana, nafikiria siku ambayo ulikwenda…”

Muhtasari

• Miezi mitatu iliyopita DJ Brownskin aliwakera wengi baada ya video ikionesha mkewe akinywa sumu kusambaa.

• Njeri alizikwa nyumbani kwa wazazi wake katika kijiji cha Koimbe Weithaga, Kaunti ya Murang'a, Agosti 6, 2022.

DJ Brownskin azuiliwa kwa siku 3 zaidi huku uchunguzi dhidi ya kifo cha mkewe ukiendelea.
DJ Brownskin azuiliwa kwa siku 3 zaidi huku uchunguzi dhidi ya kifo cha mkewe ukiendelea.
Image: Instagram

Mcheza santuri DJ Brownskin amemkumbuka mkewe marehemu Sharon Njeri kwa ujumbe wa kuliza akisema kwamba atazidi kumkosa sana katika pengo aliloliacha maishani mwake.

Inaeleweka kwamba Sharon Njeri alifariki Julai 29 mwaka jana lakini video ya kuonesha matukio ya ukakasi jinsi alifariki iliibuka miezi mitatu iliyopita.

Julai 29 mwaka 2023 ambayo ilikuwa wikendi iliyopita, DJ huyo maarufu wa Reggae hakuacha siku hiyo ipite tu.

Alipakia picha ya mshumaa uliowashwa kwenye Instastory yake akiambatanisha picha hiyo ya wimbo wa msanii P Diddy aliomshirikisha Faith Evans, kwa jina ‘I’ll be Missing You’.

Wasanii hao walitoa wimbo huo kama njia moja ya kumukumbuka na kuuenzi msanii wa rap maarufu Notorious B.I.G lakini DJ Brownskin aliutumia vile vile kumkumbuka na kumuenzi mkewe Sharon Njeri.

“Ndio huu wimbo hapa unaendea kila mmoja aliyempoteza mpendwa wake, ambaye alikuwa anampenda sana… ni kama tu jana tulikuwa tunafunika shoo pamoja,.. maneno hayawezi kuelezea maana yako kwangu, hata kama umekwenda sisi wote bado ni timu moja… katika maisha ya mbeleni sitosubiri kukuona tena kama utanifungulia milango. Siwezi tafakari uchungu ninaopitia na nitatoa kitu chochote ili kusikia kupumua kwako, najua bado unaishi maisha yako hata baada ya kufa…nitakumiss sana, nafikiria siku ambayo ulikwenda…” sehemu ya mistari kwenye wimbo huo inaimba.

Miezi mitatu iliyopita siku ya wikendi kama Jana, DJ Brownskin aliwakera Wakenya wengi baada ya video ya mkewe akinywa sumu huku mcheza santuri huyo anamwangalia tu akimrekodi na kumshabikia kujitoa uhai kusambaa.

Katika video hiyo ya ukakasi ambayo baadae DCI walibaini kwamba ilivujishwa na mchepuko wa DJ huyo anayeishi nje ya nchi, DJ alimrekodi mkewe akinywa kile kilichosemekana kuwa ni sumu na hakuonekana kuchukua hatua yotote ya kumzuia kutojiua.

Baadae alisemekana kumtumia mpenzi wa kando video hiyo akimwambia kwamba mkewe ameshafariki na hata kumtaka sasa kuanzisha mapenzi naye kwa njia huru.

Njeri alizikwa nyumbani kwa wazazi wake katika kijiji cha Koimbe Weithaga, Kaunti ya Murang'a, Agosti 6, 2022.