Harmonize adai kila mtu anasubiria remix ya Single Again na Ruger, wimbo mkubwa 2023

Msanii Diamond aliwafungulia wenzake pazia kwa kufanya kolabo ya My Number One na Davido, wimbo ambao kwa asilimia kubwa ndio ulimtambulisha Diamond kwenye majukwaa makubwa ya ulimwengu.

Muhtasari

• "Msitufanyie cha mwaka jana hakuna wimbo mkubwa tangu mwaka huu unaze kushinda Single Again Remix" - Harmonize.

Harmonize
Harmonize
Image: Instagram

Msanii wa kizazi kipya kutoka Tanzania ametupa jiwe gizani akidai kwamba wasanii wengine kina Alikiba na Harmonize wanafaa kuacha kutamba kwamba wametoa nyimbo kubwa mwaka huu wa 2023.

Kupitia Instagram story yake, Harmonize amedai kwamba kila msanii ndio mwanzo ameketi kitako akisubiria wimbo wake mkubwa wa Single Again ambao ni remix aliyoshirikisha Ruger kutoka Nigeria.

Harmonize alipigia debe remix hiyo inayotarajiwa kutoka Kesho Ijumaa akisema kwamba ndio wimbo pekee mkubwa ambao utashuhudiwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kauli hii ililenga kumgonga Alikiba ambaye juzi alikwenda Twitter na kutamba wazi wazi kwamba wimbo wake wa Mahaba ndio huenda wimbo wa pekee kuwa mkubwa mwaka huu baada ya kugonga Zaidi ya streams milioni 34 kwenye Boomplay ndani ya miezi 5.

“Single Again Remix ndio kolabo kubwa zaidi Afrika Mashariki na Magharibi kuwahi kutokea mwaka 2023. Tilia maanani kidogo kwa sababu hii imeenda. Msitufanyie cha mwaka jana hakuna wimbo mkubwa tangu mwaka huu unaze kushinda Single Again Remix, kwa hiyo acha tuichukue kule Billboard,” Harmonize alitamba.

Msanii huyo alitaja Ijumaa kuwa siku moja ya kihistoria katika muziki wa Bongo Fleva.

“Mungu wangu nafikiria ni nini cha ajabu ambacho nitakifanya. Sijawahi kuwa katika klabu,” alisema huku akiwataka maDJ wote duniani kuukumbatia wimbo huo na kusema kwamba anatambua mchango wao na ndio watakaoufanikisha wimbo huo kuwa mkubwa.

Licha ya kudai kwamba yeye ndiye msanii wa kwanza kufanya collabo ya Mashariki na Magharibi mwa Afrika kuwa mkubwa, tuliweza kurudi kwenye makabrasha na kupekuwa kuona wasanii waliowahi kuanya kolabo kubwa.

Msanii Diamond aliwafungulia wenzake pazia kwa kufanya kolabo ya My Number One na Davido, wimbo ambao kwa asilimia kubwa ndio ulimtambulisha Diamond kwenye majukwaa makubwa ya ulimwengu.

Mwenzake Alikiba pia alifanya collabo na Mayorkun bila kumsahau Jux aliyefanya wimbo na msanii wa kike kutoka Ghana miongoni mwa wengine.