Kibe adai wanaume kwenye ndoa huharibikiwa na tumbo kwa kulishwa steelwool na wake

“Unapata nyumbani mke amenuna amekuchanganyia steelwool kwenye chakula hajawai acha kuhara kila siku, unapoteza uzani wa mwili ni kama mtu wa kutumia dawa za kulevya anashangaa ni nini."

Muhtasari

• Mwanablogu huyo alishauri kwamba kwa mwanamume yeyote ambaye yuko katika ndoa, ni sharti alale kama amefungua jicho moja.

Andrew Kibe
Andrew Kibe
Image: Screengrab

Mwanablogu wenye utata katika mtandao wa YouTube Andrew Kibe anahisi kwamba wanaume wengi ambao huharibikiwa na tumbo mara kwa mara kusababisha kuharisha ni wale walioko katika ndoa.

Kibe katika podikasti yake alitoa maoni kwamba wanaume wengi katika ndoa huharibikiwa na tumbo kutokana na chakula chenye madini hatari ambacho wake zao huwapikia pindi wanapowakosea.

“Unapata nyumbani mke amenuna amekuchanganyia steelwool kwenye chakula hajawai acha kuhara kila siku, unapoteza uzani wa mwili ni kama mtu wa kutumia dawa za kulevya anashangaa ni nini. Wewe umeenda umekasirisha mke na yeye ndiye anapika chakula. Kila siku anaingia jikoni anaambia watoto ‘msikule chakula cha baba, hicho ni spesheli’ na ukija anakupakulia anaketi hapo akikushangilia ukila, mpaka unatupigia picha unatuwekea kwenye mitandao lakini kuhara nayo…” Kibe alisema.

Mwanablogu huyo alishauri kwamba kwa mwanamume yeyote ambaye yuko katika ndoa, ni sharti alale kama amefungua jicho moja kwa kile alisema kuwa wanawake ndio adui wakubwa kwa wanaume kaitka ndoa.

Alisema kwamba mwanamume yeyote ambaye anaharibikiwa na tumbo kutokana na chakula anafaa jambo la kwanza kufanya ni kufanyiwa vipimo vya damu ili kuona madini hatari ambayo yamejazana na pia kukoma kula chakula cha nyumbani.

“Ukiwa mtu umeoa kitu cha kwanza lazima ulale na jicho moja ukiwa umefungua. Nasema ukiwa unaharibiiwa na tumbo mara kwa mara, acha kula chakula cha nyumbani na kitu cha pili nenda ukafanyiwe vipimo vya damu. Utapata unakula kufuli nyingi,” Kibe alishauri.

Kibe alisema kuwa wanawake si watu wa kusahau haraka na kila mwanamume anapowakosea huwa wanaweka kitu hicho kwenye kichwa chao na kuja kukulipizia kwenye chakula.

Unakubaliana na maoni ya Kibe?