Edday Nderitu adai mwanamke anayemuiga kama mfano ni Lucy Kibaki

“Lucy kibaki my hero💪kwanza Ile part she made kibaki Tu kutangaza ana mke mmoja tu,” Mama Boys alimwambia huku Edday akimjibu kwamba, “Alikuwa ni mwanamke wa nguvu sana.”

Muhtasari

• Edday Nderitu aliondoka Kenya kwenda Marekani miezi kadhaa iliyopita katika kile kilichoonekana kama ni ziara ya miezi michache na kurudi nchini.

Edday Nderitu.
Edday Nderitu.
Image: Facebook

Edday Nderitu, mke wa msanii wa mugithi Samidoh amefichua kwa mashabiki wake kuwa mwanamke ambaye anamuiga kama kielelezo bora ni aliyekuwa mama wa taifa Lucy Kibaki.

Nderitu alipakia video fupi katika ukurasa wake wa TikTok akinywa sharubati ambapo alidokeza kwamba amemkosa sana mwanamke kielelezo chake – Lucy Kibaki.

“Leo sikuwa na dhamira la kunywa lakini wanaume tu! Ni vile nimemkosa kielelezo changu Lucy Kibaki,” Nderitu aliandika kwenye video hiyo.

Katika upande wa kutoa maoni, rafiki yake mkubwa Bernice Saroni ambaye anajiita Mamake Boys alimjibu akisema kwamba kitendo anachokitambua kutoka kwa mama huyo wa taifa ambaye hakutaka mchezo wa wanawake karibu na mume wake ni kile cha kumshurutisha Kibaki kuita mkutano na wanahabari kutangazia umma kwamba ni yeye mke wake wa kipekee wala hakuna mwingine.

“Lucy kibaki my hero💪kwanza Ile part she made kibaki Tu kutangaza ana mke mmoja tu,” Mama Boys alimwambia huku Edday akimjibu kwamba, “Alikuwa ni mwanamke wa nguvu sana.”

Baadhi ya watu waliofika kwenye chapisho hilo walihisi huo ni uchokozi wa moja kwa moja kwa msanii Samidoh ambaye kwa sasa anaongozana na mama watoto wake Karen Nyamu baada ya kuondoka kwa Edday Nderitu.

Edday Nderitu aliondoka Kenya kwenda Marekani miezi kadhaa iliyopita katika kile kilichoonekana kama ni ziara ya miezi michache na kurudi nchini.

Lakini wiki mbili zilizopita aliwashangaza wengi baada ya kudokeza kwamba hatimaye amefaulu kuwaweka watoto wake katika mfumo wa masomo ya Marekani, jambo ambalo lilitoa ishara wazi kwamba mama huyo wa watoto watatu hana mpango wa kuwarudisha watoto kwa baba yao Samidoh muda wowote hivi karibuni.