Tangu nizaliwa nimekuwa na mwanaume mmoja tu na ndiye atanioa - Maua Sama

Sama anazua suala la usichana ikiwa ni siku chache tu baada ya msanii mwenzake wa kike Zuchu kudai kwamba tangu azaliwe amelala kimapenzi na mwanamume mmoja tu – Diamond.

Muhtasari

• Sama aliandika hayo na kusema kwamba hivi karibuni watafunga harusi pamoja na mwanamume huyo aliyemtaja kama mpenzi wake wa kwanza.

Maua Sama
Maua Sama
Image: Insta

Malkia wa Bongo Fleva Maua Sama amezua mjadala katika mtandao wa Twitter baada ya kudai kwamba tangu azaliwe hajawahi toka kimapenzi na mwanamume mwingine Zaidi ya yule aliye naye sasa hivi.

Sama aliandika hayo na kusema kwamba hivi karibuni watafunga harusi pamoja na mwanamume huyo aliyemtaja kama mpenzi wake wa kwanza.

“Kutoka nizaliwe sijawahi kuwa na mwanamume mwingine zaidi ya mwanamume wangu wa sasa, siwezi subiri kufunga harusi na yeye, mpenzi wangu wa kwanza,” Sama aliandika.

Baadhi ya mashabiki wake walionekana kupingana na kauli hiyo yake wakisema kuwa huenda ni kweli hajawahi kuachana na mwanamume huyo lakini hiyo haimaanishi kwamba hajawahi chepuka na wengine.

“Unajua hata mimi tangu nizaliwe nimewahi kuwa na baiskeli MOJA TU lakini hizi za kuazima unapanda kupiga nazo round kisha naachana nazo, ah! Mbona nyingi tu! Can't wait using motorcycle tires in my bicycle!” mmoja alimtania.

“Unaķosa mengi sana pole” mwingine alisema.

“Kwaiyo we dada unataka kutuambia ndo aliyekutoa ugoko...” aliulizwa.

Sama anazua suala la usichana ikiwa ni siku chache tu baada ya msanii mwenzake wa kike Zuchu kudai kwamba tangu azaliwe amelala kimapenzi na mwanamume mmoja tu – Diamond.

Zuchu alisema hata katika kipindi cha maswali na majibu na Wasafi FM alipoulizwa swali hilo na kusema kuwa ni Diamond pekee ndiye aliyemtoa ubikira.