Abigail Chams asema chombo chake bado hakijapigwa

Ameeleza kuwa tendo la ndoa ni takatifu na linatoka kwa mwenyezi Mungu , hivyo si jambo la kufanya kiholela bila mpango

Muhtasari

•Kwenye mazungumzo yake ya moja kwa moja na  kituo cha redio cha clouds fm,arusha Tanzania,alikiri kwamba hajawahi kwa maisha yake kufanya tendo la ndoa mpaka kufikia hapa alipo.

Abigail Chams/Instagram
Abigail Chams/Instagram

Abigail Chamungwana anayejulikana sana kana Abigail Chams, ni mcheza ala za muziki na mwanaharakati wa kijamii anayetokea Kilimanjaro,Tanzania

Kwenye mazungumzo yake ya moja kwa moja na  kituo cha redio cha Clouds fm,arusha Tanzania, alikiri kwamba hajawahi kwa maisha yake kufanya mapenzi.

Amesema kwamba hajawahi kumpenda au kupata mtu anaye muita mpenzi. Mahusiano ya pekee ambayo amewahi kujihusisha nayo kulingana na yeye yalidumu kwa  muda wa siku mbili .

"Mimi ni mtu ambaye sijawahi kupenda wala kufanya tendo la mapenzi,ila ninapoona jinsi wazazi wangu wanvyopendana, natamani, ila najua siku moja nitapenda."

Alisisitiza kuwa hajawahi kushiriki tendo la ndoa tangu azaliwe,

"Sijawahi kuwa na mahusiano,ila nakumbuka ikiwa kuna mahusiano nimewahi jihusisha ni yale ambayo yalidumu kwa muda wa siku mbili tu, na hilo silichukulii kama uhusiano."

Chams ameeleza kuwa tendo la ndoa ni takatifu na linatoka kwa mwenyezi Mungu , hivyo si jambo la kushiriki kiholela  bila mpango wa baraka kwani linaitaji kufanyw na watu ambao wamefunga pingu za ndoa.

Anasema ni wengi wanaotaka mahusiano naye ila amebaki na msimamo wake wa kusalia kuwa bikira mpaka pale atakapopata mtu wa kuchumbiana naye wa kuingia naye katika ndoa.

Kipusa huyo mwenye umri wa miaka 20 sasa ana imani kuwa ipo siku atapata mpenzi atakaye shiriki naye tendo hilo wakati mwafaka utakapofika.

Abigail anafanya kazi sana ndani ya jamii kupitia kipindi chake cha vijana cha, `Teen Talks na Abby Chams`, ni programu ya vijana ambayo inalenga kuongeza ufahamu kwa vijana kusuhu afya ya kiakili ambayo inatenga nafasi kwa vijana kujieleza changamoto zinazowakabili na kutoa jawabu ya kukabiliana nazo. 

Pia ni mtetezi wa wa vijana kwa UNICEfnchini Tanzania ambao uathirika na afya ya kiakili na usawa wa jinsia.