Msiniige kwa sababu hamna nguvu sawa na mimi - Akothee

Hata hivyo amewaambia wale ambao wanajaribu kunakili kile ambacho anakifanya, wasikilize anachowaambia ila wasijaribu kumuiga.

Muhtasari

• Ameeleza kwamba yeye ni mtu wa kupigiwa mfano katika jamii kwa yale ambayo anafanya,hasa kwa wanawe na hili ninaonyesha wazi ni nini maana ya mzazi

Eshter Akothee/Instagram
Eshter Akothee/Instagram

Mwanamuziki Esther Akothee, amesema kuwa ni vigumu kwa mtu yeyote yule kuiga mitindo yake ya kutekeleza mambo.

Amesema nguvu anazotumia kutekeleza mambo yake ni ya juu ya wastani na hivyo, anaamini hakuna anayeweza kumudu kutekeleza yale ambayo anayafanya.

"Usiniige kwa sababu hauna nguvu sawa na mimi."

Ameeleza kwamba yeye ni mtu wa kupigiwa mfano katika jamii kwa yale ambayo anafanya,hasa kwa wanawe na hili ninaonyesha wazi ni nini maana ya mzazi.

"Tafathali, msiniige kwa sababu hamna nguvu sawa na mimi,na kuanzia leo mimi ni mtu wa kupigiwa mfano hasa kwa wanangu na hili linaonyesha maana ya jina mzazi."

Hata hivyo amewaambia wale ambao wanajaribu kunakili kile ambacho anakifanya, wasikilize anachowaambia ila wasijaribu kumuiga.

"Tafathali msikilizeni ninachokisema ila msininakili."

Amesema kwamba kama mzazi ili kuakikisha uko na uhusiano wema na wanao, usisusie kujadili mambo muhimu jinsi wanavyo kua,akisema anawafadhili kifedha na kuzungumza mambo muhimu ya kimapenzi.

"Ninazungumza na wanangu mambo muhimu, ninawapa pesa za kuwawezesha kujikimu,na hivyo hawajawahi kuniletea mwanaume kwa nyumba wala hawajawahi kujaribu kuavya ujauzito wowote , na wamahahidi ili mpaka watakapomaliza shule." Alisema.

Kwenye kanda ya video iliyochapichwa na Mpasho,Akothee alisisitiza haya huku akiwa na hisia akisema kwamba, kwa kisasi cha sasa mwanamke anaweza kutekeleza majumu ya familia ikiwa tu atajijushughulisha kwa heshima na kwa kuwajibika.

Ameshawishi wale ambao wangetaka kuwa wanawake wenye kuwajibika na wenye heshima,kujiita mkutano na kuwaza jinsi ya kuendelea na kusonga mbele na kuheshimika kwa jamii.