Tanasha Donna aonekana katika nyumba ya Diamond - video

Machi mwaka huu, Tanasha alionekana kwenye video akiwa nyumbani kwake akiwa na mtoto wao wa kiume.

Muhtasari

• Tanasha amekosekana mtandaoni kwa zaidi ya miezi miwili

• Video imetoka kwa mama Diamond

amemsherehea mamake na kumpuuza baby mama wake Tanasha Donna
Diamond Platnumz amemsherehea mamake na kumpuuza baby mama wake Tanasha Donna
Image: INSTAGRAM

Mrembo wa Kenya Tanasha Donna amekuwa  akikokosekana kwa  mtandao kwa muda mrefu sana jambo ambalo imeimbua hisia kwa mashabiki wake.

Kutokuwepo kwake kumezua wasiwasi kutoka kwa mashabiki wanaohitaji kujua aliko. Mama Dangote ameweka  video ya Tanasha na mwanaye Naseeb nyumbani kwa mwimbaji huyo wa Bongo Tanzania.

Video ambayo haijawekwa tarehe hata hivyo imewasisimua mashabiki na kuwafurahisha kuona jinsi mtoto wa Diamond alivyo mzuri.

Naseeb Junior mtoto wa Diamond na kufanana kwao mara nyingi humfurahisha mwimbaji huyo.

 Katika video hiyo (chini kwa hisani ya Instagram), Tanasha anamhimiza mwanawe kusema kwa sauti 'Asalam Alaikum".

Anamfuraisha mama yake na matamshi yake ni ya kupendeza. Haijabainika ikiwa hii ni video ya sasa ya mwimbaji huyo wa Kenya, kwani mamake Diamond, Sandra anazungumzia tu jinsi moyo wake unavyochangamka kwa kijana huyo.

Tanasha amekuwa aonekani kutoka kwa mtandao wake wa kijamii kwa karibu miezi miwili. Picha ya mwisho aliyoshiriki ilikuwa ya picha zake za siku yake ya kuzaliwa akiwa na umri wa miaka 28. Mnamo Mei, Tanasha alikasirishwa na matukio nchini Kenya alipendekeza kuwa anaweza kuhama.

Machi mwaka huu, Tanasha alionekana kwenye video akiwa nyumbani kwake akiwa na mtoto wao wa kiume. Amelala kwenye sofa akimkumbatia mwanae, huku tukimuona Diamond kwenye sofa lingine akiwa  pia kwenye simu yake.