TikToker MtumbaMan alia kuchapwa na mpenziwe, aonyesha jinsi alichezea kichapo - video

"Napitia kuzimu lakini siwezi kuzungumza juu yake kwa sababu jamii inaamini wanaume wana nguvu na wanaweza kushinda kila hali." alinukuu video hiyo.

Muhtasari

• ”Nimechoka naapa nimechoka Mungu tafadhali ipo siku ill be no more because am too good to people around me." alisema.

• Kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 alisema kwamba alilelewa vizuri akionyesha kwamba hatawahi kuweka mikono yake juu ya mwanamke.

Mtumba Man.
Mtumba Man.
Image: Insta

TikToker Mtumba Man ni mwanamume wa hivi karibuni ambaye ameangukia mkono wa kichapo kutoka kwa mpenzi wake wa kike katika msururu wa ukatili wa kinyumbani ambo umekuwa ukiwakumba wanaume.

Akishiriki video yake akiwa amevalia shati jeusi lililochanika, mwanamume huyo mcheshi alionyesha simu iliyovunjika, kidole kinachovuja damu na majeraha kwenye eneo la shingo yake. Alimshutumu mpenzi wake kwa kumsababishia majeraha hayo.

MtumbaMan alieleza kuwa amekuwa akipitia unyanyasaji huo kwa muda mrefu lakini hakuweza kushiriki mateso yake kwa sababu ya kuogopa hukumu kutoka kwa jamii.

"Napitia kuzimu lakini siwezi kuzungumza juu yake kwa sababu jamii inaamini wanaume wana nguvu na wanaweza kushinda kila hali. Ni Mungu pekee ndiye anayeweza kunisikiliza coz wengi wenu mtasikiliza, mtacheka, mtatia huruma, na hata hizi zitajirudia tu.” mchekeshaji huyo alichapisha kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 alisema kwamba alilelewa vizuri akionyesha kwamba hatawahi kuweka mikono yake juu ya mwanamke.

”Nimechoka naapa nimechoka Mungu tafadhali ipo siku ill be no more because am too good to people around me. Nililelewa vizuri lakini wanadamu wanaweza kukubadilisha,” alinukuu video yake.

Itakumbukwa pia miezi kadhaa iliyopita mchekeshaji mwenza 2Mbili aliibuka mitandaoni akikiri kwamba anapitia wakati mgumu kutokana na kudhulumiwa na mama wa watoto wake.