"Usikimye katika mahusiano ya dhuluma, kimbia!" Watu mbalimbali wamuomboleza Osinachi

Muhtasari

• Nchini Kenya, watu mbalimbali Jumapili walichukua mitandaoni kuonesha kero zao kwa kile walisema kwamba ni jambo la kuhuzunisha kuwa Osianchi, msanii mkubwa tena tajika uhai wake ulikatishwa mikononi mwa mwanaume dhalimu.

Image: Gloria Muliro, Melody Sinzore, Sammy Ondimu Ngare (Facebook)

Wikendi iliyopita, ulimwengu ulikaribisha taarifa za huzuni na tanzia kuhusu kifo cha mwimbaji wa injili mashuhuri kutoka nchini Nigeria kwa jina Osinachi.

Mwimbaji huyo mwenye sauti ya ninga aliyoitumia vizuri kwa kufanya tungo kadha za kumtukuza Mungu alifahamika pakubwa tena kote duniani kwa kibao chake cha ‘Ekwuweme’ ambacho japo alikitunga kwa lugha ya Igbo ambayo ni mojawapo ya lugha yenye wazungumzaji wengi nchini Nigeria, lakini kibao hiki kilipata mapokezi makubwa na ufanisi wa kihistoria kote duniani.

Awali, watu wengi waliokuwa wakimshabikia mwinjilisti huyo hawakufuatilia kwa kina sana kujua kiini cha kifo chake kwani butwaa la taarifa za kifo chenyewe ziliwafunika macho wengi mpaka kusahau kuuliza kilichosababisha kifo.

Baadae taarifa za kukwaza mno ziliibuka kutoka kwa Rafiki za mwanamama Osinachi kwamba kifo chake kilisababishwa na kudhulumiwa na mumewe kwa manyanyaso ya kinyumbani.

Suala hili la kuvunja moyo lilipokelewa kwa nyoyo za kuvunjika mno ambapo mitandao ya kijamii iliwaka moto kwa kashfa dhidi ya vita na dhuluma katika ndoa, ambazxo kwa mara nyingi wanaumia zaidi kutokana na mizozo hiyo katika ndoa ni wanawake.

Nchini Kenya, watu mbalimbali Jumapili walichukua mitandaoni kuonesha kero zao kwa kile walisema kwamba ni jambo la kuhuzunisha kuwa Osianchi, msanii mkubwa tena tajika uhai wake ulikatishwa mikononi mwa mwanaume dhalimu.

Chungu zaidi ni kwamba aliwahi shauriwa kuachana na ndoa hiyo ya kidhalimu ambapo alifanyqa jaribio la kutoka lakini mhubiri wa kanisa lake akawasuluhisha na mumewe ambaye ni kiongozi mkuu kanisani na kuwarudisha pamoja kwa kisingizio kwamba Mungu hapendi talaka!

“Moyo wangu unavuja damu kwa ajili ya nafsi hii. Mtumishi wa Mungu Osinachi, Pumzika. Wanawake! Wanaume! Je, ikiwa aibu ya “watasema nini…” uponyaji wako umejificha? Sikiliza, je maisha yako yako hatarini? USISUBIRI KUFA!” Mwimbaji Gloria Muliro aliomboleza.

“USIKAE KWENYE NDOA YA MATUSI au MAHUSIANO. USIFANYE! KUANDIKA RIP HAITAKURUDISHA AU KUWAPONYA WAPENZI WAKO UKIFA,” Mtangazaji Melody Sinzore aliandika pia.

“Ikiwa uko kwenye ndoa yenye unyanyasaji, una chaguo moja tu la mwisho... KIMBIA. Umewashirikisha wazazi wote na mtu habadiliki.. Rafiki yangu una chaguo moja tu........ KIMBIA. Umehusisha wachungaji, marafiki, wafanyakazi wenzako na haifanyi kazi, una chaguo moja........KIMBIA. Masuala ya ndoa hayawezi kutatuliwa na polisi..rafiki yangu kipenzi..... KIMBIA. Mimi ni Baba wa wasichana Watatu, nitawaambia kila mara wakimbie nyumba za matusi...Binti yangu atabaki kuwa wangu hata akiolewa…USISUBIRI MPAKA UFE. UNA CHAGUO MOJA LA MWISHO... KIMBIA KIMBIA NA UKIMBIE. SEMA HAPANA KWA UKATILI WA NDANI YA NDOA,” aliomboleza pia polisi maarufu Sammy Ondimu Ngare.