Densi ya Crazy Kennar wakiwa na Bibiye yaibua hisia mseto mitandaoni

Wote wawili walivalia miwani ya jua iliyopendeza, na kilichofuata ni densi ya ghafla

Muhtasari

•Video hiyo iliyorekodiwa katika kijiji chake cha Awasi, Kaunti ya  Kisumu, imewafurahisha watumiaji wa mtandao, na kujipatia sifa kwa mchanganyiko wake wa ucheshi na moyo.

Crazy Kenner wakiwa na Bibiye
Crazy Kenner wakiwa na Bibiye

Crazy Kennar, mmoja wa waundaji maudhui wanaopendwa zaidi nchini Kenya, amewafurahisha mashabiki wake kwa video ya kupendeza iliyoonyesha kipaji chake cha ucheshi na mshirika wa kustaajabisha wa dansi, bibi.

Video hiyo iliyorekodiwa katika kijiji chake cha Awasi, Kaunti ya  Kisumu, imewafurahisha watumiaji wa mtandao, na kujipatia sifa kwa mchanganyiko wake wa ucheshi na moyo.

Katika video hiyo, mtayarishaji wa maudhui alionekana akielekea kwenye kamera huku bibi huyo mzee akikaribia kutoka upande mwingine.

Wote wawili walivalia miwani ya jua iliyopendeza, na kilichofuata ni dansi ya ghafla.

Mcheshi na bibiye wanaonyesha miondoko yao ya densi kwa mtindo wa kusisimua. Kilichovutia zaidi ni uhodari wa densi wa bibi kizee huyo.

Bibiye Kennar alidhibitisha kwamba umri ni namba tu linapokuja suala la kufurahia maisha na kujiburudisha,umri aujalishi.

Baadhi ya mashabiki waliofurahishwa na kucheza kwa bibiye,walitoa maoni na hisia tofauti tofauti.

Baadaye wawili hao walipigwa picha za kupendeza ambazo muundaji maudhui huyo alichapisha kwa mitandao na kupata hisia tofauti kutoka kwa mashabiki wake wanomfuatilia.

Awali mcheshi huyo alichapisha video kwenye ukurasa wake akiwaambia mashabiki wake wawe tayari kwa shoo ambayo amathamiria kuifanya mnamo disemba mwaka huu.

Kwenye video hiyon aliwasihi mashabiki wake wazidi kumpiga jeki ili kufanikisha mradi huo ambao anapanga kuanziasha wa burudani.