Nadia Mukami asimulia safari yake Marekani kwa Tuzo ya AFRIMMA

Mwanamuziki Nadia Mukami amerejea nchini baada ya safari yake Marekani

Muhtasari

•Nadia alishinda kitengo cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki, akiwashinda wasanii wenzake kama Zuchu wa Tanzania miongoni mwa wengine.

•  Mwanamuziki huyu pia  anatazamiwa kuingia mwezi ujao na wateule wengine baada ya kuteuliwa katika tuzo za mwaka huu za TRACE Continental zitakazofanyika Kigali, Rwanda mwezi Oktoba

 

Nadia Mukami.
Nadia Mukami.
Image: Instagram

Mwanamuziki Nadia Mukami amerejea nchini baada ya safari yake Marekani baada  kusafiri  kuhudhuria tuzo za AFRIMMA 2023.

Mshindi huyu wa kike alizuru marekani ambapo sherehe za kutuzwa tuzo ili zilifanyika huku akishabikiwa sana wa kuwa msanii pekee wa kike Afrika Mashariki.

Baada ya kufika uwanja wa JKIA mshindi huyu alikaribishwa kwa shagwe na wafuasi wake akiwemo mpenzi wake ambaye pia ni mwanamuziki nchini Kenya.

"Nafuraishwa sana na ushindi wangu safari yangu ilikuwa ya mafanikio nimerudi nyumbani na Tuzo jambo ili linanitilia moyo nilikutana na marafiki wangu Marekani wengi wakanipa zawadi tofauti nashukuru mwenyenzi Mungu na familia yangu kwa kunishika mkono".alisema Nadia.

Nadia alishinda kitengo cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki, akiwashinda wasanii wenzake kama Zuchu wa Tanzania miongoni mwa wengine.

Baada ya mahojiano na wanablogu Nadia amesimulia safari yake akisema kuwa akutembea na familia yake jambo ambalo limemfanya kurudi nchini haraka .

"Ninahisi kama Kipenzi cha Mungu kwa sababu nilijitahidi kwa miezi kadhaa na nilichukua video za muziki na picha kwa Ujumla! Namshukuru Mungu kwa upendo wake usio na masharti na kwa kunipa kila wakati vitu vitatu! Neema, Rehema na upendo".mwanamuziki huyu alisema.

   Nadia pia  anatazamiwa kuingia mwezi ujao na wateule wengine baada ya kuteuliwa katika tuzo za mwaka huu za TRACE Continental zitakazofanyika Kigali, Rwanda mwezi Oktoba.

Nadia Mukami.
Nadia Mukami.
Image: Instagram