Omanyala atimba studioni kurekodi wimbo wa shukrani kwa Mungu

Mashabiki wake wlimpongezi kwa kuonesha weledi na umahiri wake si tu katika mbio bali pia katika kumuimbia Mungu.

Muhtasari

• “Kutafakari jinsi Mungu amekuwa mkuu. Kuwa na muda na Mungu kupitia ibada,” aliandika kwenye video hiyo.

• “Naomba Collabo,” Msani na mtangazaji wa kipindi cha injili kwenye runinga ya Citizen Timeless Noel alimtania.

Omanyala.
Omanyala.
Image: Insta

Mshikilizi wa rekodi ya kutimka kwa mbio Zaidi katika mbio za mita 100 barani Afrika, Mkenya Ferdinand Omanyala ametimba studioni kurekodi wimbo wa kurudisha shukrani zake kwa Mungu.

Omanyala ambaye hajakuwa akifanya vizuri katika siku za hivi karibuni katika msimu wa raidha za dunia ambao umekamilika juzi alionekana akiwe kwenye studio huku amevalia visikizi masikioni na mbele yake kinasa sauti.

Kwa mdundo wa taratibu, Omanyala alitoa moyo wake kwa sauti nzuri ya wimbo wa kuabudu huku akiimba tenzi ya rohoni, “Unastahili kuabudiwa, unastahili eewe Yesu, Unastahili kuabudiwa…”

Kwenye kapsheni ya klipu hiyo ya kutia moyo, Omanyala ambaye ni afisa wa polisi alisema kwamba kilichomchechea kuingia studioni kufanya zoezi la kuimba ni kupiga tafakari ya umbali ambao amekuwa akishikiliwa na Mungu tangu aingie kwenye mbio rasmi na kujijengea jina katika mashindano ya Olimpiki jijini Tokyo Japan mwaka juzi.

“Kutafakari jinsi Mungu amekuwa mkuu. Kuwa na muda na Mungu kupitia ibada,” aliandika kwenye video hiyo.

Mashabiki wake walimtania wengine wakimuomba Kolabo na wengine wakimpa pongezi kwa kukumbuka kwamba yote ambayo amekuwa akiyafanya uwanjani si kwa uwezo wala nguvu zake bali ni za Muumba wake.

“Naomba Collabo,” Msani na mtangazaji wa kipindi cha injili kwenye runinga ya Citizen Timeless Noel alimtania.

“Na Mungu anafurahi !!! Si wengi hutie there success to God in the athletics world..but wewe ni mrare....Sasa ngoja uone venye God atakam through... imagine hata Badoo hajaanza kukubless 😂😂..ndio mwanzo,” Wabwire is Innocent alimwambia.

“Sio bingwa tu bali pia Mcha Mungu na Kumwabudu ... Wow 💥💥” Huruma Town80.

“kumbe wewe ni Muimbaji pia! Mungu ni mwema na anastahili utukufu 🙏🏾” Kiki G Kinyua.

“Asante kwa kumtambua Mungu, atakuchukua mahali unapomwacha achukue utukufu. 🙌🙌❤️❤️ Endelea kubarikiwa kaka na tunajivunia wewe,” Ann Wanja.

Omanyala alishindwa vibaya Zaidi katika mashindano ya dunia ya Budapestmwishoni mwa mwezi Agosti kwa kumaliza mbali katika nafasi ya 7.