Mama Dangote afunguka, atamani Diamond aoe lakini hajafanikiwa

Msanii Diamond kwa sasa hajafanikiwa kuwa na ubavu wake wa kudumu

Muhtasari

•Natamani mwanangu Diamond aoe hata kama ni sasa hivi ila lakini huenda yeye hajafanikiwa kupata  ama labda mwenyezi mungu hajampa ubavu wake ila kila siku namwambia mwanangu  Naseeb oa mpaka wakati mwingine nawatuma marafiki na dada zake waongee naye

Image: INSTAGRAM// MAMA DANGOTE

Furaha ya Mzazi ni kuona wanae  wakifanikiwa kwa kila jambo wafanyao kwa maisha ila  kwa sasa Mama Dangote amejawa na kiu ya kuona mwanae Diamond akifanikiwa kwa Ndoa

Licha ya kuwa nyota wa muda mrefu  wa nyimbo za Bongo  msanii Diamond kwa sasa hajafanikiwa kuwa na ubavu wake wa  kudumu baada ya kusabaratika kwa mahusiaono  ya mapenzi dhidi ya  Zari Hassan,Wema sepetu ,Tanasha Donnah na wengine ambao walichumbiana kwa muda.

Jambo ambalo linamtatiza Mama Dangote ambaye ni mamake mzazi aliyefunguka jambo hili  kwenye mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha Radio Wasafi FM .

"Natamani mwanangu Diamond aoe hata kama ni sasa hivi ila lakini huenda yeye hajafanikiwa kupata  ama labda mwenyezi mungu hajampa ubavu wake ila kila siku namwambia mwanangu  Naseeb oa mpaka wakati mwingine nawatuma marafiki na dada zake waongee naye ."alisema .

Diamond kwa sasa kwenye mitandao duru zinaarifu kuwa huenda wanachumbiana na Zuchu ambaye ni mmoja wa wasanii waliosajiliwa chini ya mwavuli  Wasafi Records WCB.

Ila mapenzi haya kulingana wabebesi yanakubwa na matatizo kwa kile wanachodai Diamond kuwa karibu sana na mtoto wa aliyekuwa mpenzi wake Tanasha Donnah