Alikiba adaiwa kupata mrembo mpya na kumhonga kwa gari, ampost kwenye Instagram

Lakini kilichowazuzua wengi ni hatua ya msanii huyo kumuita ‘Mpenzi’, licha ya kuwa ni nadra sana kwake kupakia picha ya mwanadada kwenye kurasa zake za mitandaoni.

Muhtasari

• Mrembo huyo Babi Sherrie ni vixen wa video na alicheza katika wimbo wa msanii huyo wa So Hot.

Alikiba na mrembo mpya.
Alikiba na mrembo mpya.
Image: Instagram

Msanii wa muda mrefu wa Bongo Fleva Alikiba amedaiwa kupata mpenzi mpya huku kukiwa na songombingo katka ndoa yake na mkewe mkenya Amina Khelef.

Alikiba ambaye si muongeaji sana alipakia picha ya mrembo huyo na kufichua jina lake huku akimsherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa makopa na kumuita ‘mpenzi’.

Mrembo huyo Babi Sherrie ni vixen wa video na alicheza katika wimbo wa msanii huyo wa So Hot.

Lakini kilichowazuzua wengi ni hatua ya msanii huyo kumuita ‘Mpenzi’, licha ya kuwa ni nadra sana kwake kupakia picha ya mwanadada kwenye kurasa zake za mitandaoni.

“Babe Sherrie, heri njema ya kuzaliwa mpenzi,” Alikiba aliandika.

Alikiba
Alikiba

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki walikwenda mitandaoni na kufichua kwamba tayari Alikiba ameshamtunuku mrembo huyo gari aina ya IST na kwake amenata.

Baada ya picha hiyo kuchochea joto mitandaoni, Alikiba aliifuta na hakuna tamko lingine ambalo limetoka kwenye kambi yake.

Itakumbukwa mkewe Alikiba, Amina Khelef amekuwa akimstumu msanii huyo kwa kile anadai kwamba amekataa kumweka huru kwa kumpa talaka yake licha ya penzi lao kuvunjika Zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Alikiba mwenyewe alipoulizwa kuhusu kudinda kumpa mkewe talaka yake, alisema kwamba ndoa ni yake na ana suluhisho kuhusu ukakasi wote lakini pia akadokeza kwamba ni jambo dogo sana ambalo haliwezi kumshinda kiasi kwamba aambiwe cha kufanya na mashabiki.