"Mimi ni kama wewe tu ni vile najua kuchora!"- Nyamu amjibu shabiki

“Hapa nilikua na balance machozi after kuwachwa na ndege ya mwisho, ndege ya safari ya usiku!”

Muhtasari

•Nyamu alijipata katika hali hii wakati shabiki alipoona viatu vyake vilivyoonekana kuwa vya bei nafuu kwenye picha aliyoweka,ambayo Nyamu alisema ilimkumbusha mbali.

• "Mhesh anavaa sandals za 500 kama Mimi tuu?"

Karen Nyamu/Instagram
Karen Nyamu/Instagram

Karen Nyamu amjibu shabiki aliyemuuliza kwa nini alivalia champali za shilingi 500,baada ya Nyamu kuchapisha picha kwenye ukurasa wake wa Instagramu akiwa kwa uwanja wa ndege.

“Yaani mhesh anavaa sandals za shilingi 500 kama mimi tu? Shabiki huyo aliuliza Nyamu.

Nyamu alijipata katika hali hii wakati shabiki alipoona viatu vyake vilivyoonekana kuwa vya bei nafuu kwenye picha aliyoweka,ambayo Nyamu alisema ilimkumbusha mbali.

Aliambatanisha picha hiyo na ujumbe wa kumbukumbu akisimulia hisia zake alipoachwa na ndege.

“Hapa nilikua na balance machozi after kuwachwa na ndege ya mwisho, ndege ya safari ya usiku!” Alisema.

Karen alikuwa na mwonekano wa kawaida na maridadi, akiwa na viatu  ambavyo, kulingana na shabiki huyo makini, vilionekana kuwa na thamani ya shilingi 500.

 Wakati ambapo lebo za mitindao ya hali ya juu na vifaa vya kifahari mara nyingi hutawala mitandao ya kijamii, maoni ya shabiki yanaweza kuwashangaza wengine.

Shabiki alishindwa kujizuia kuuliza, "Mhesh anavaa sandals za 500 kama Mimi tuu?"

Karen, ambaye anajulikana kwa akili zake za haraka na kushiriki katika mitandao ya kijamii. aliamua kushughulikia maoni kwa mguso wa ucheshi.

Akajibu akisema, "Mimi ni kama wewe tu ni vile najua kuchora!" 

Nyamu, ni mtu mashuhuri katika siasa za Kenya, si tu kwamba anatambulika kwa mafanikio yake ya kitaaluma lakini pia kwa mtindo wake wa maisha usio na wasiwasi na mtazamo mzuri wa maisha.