Natamani ndoa ila naomba itoke kwa Mungu - Zuchu

Msanii huyo kwenye mahojiano haya alisimulia kuwa wasanii wengi hupitia maneno mengi makali kwa mitandao ya kijamii.

Muhtasari

• Wanamitandao wengi ukifanya jambo zuri kamwe wanaliacha ila wakati wa jambo baya inazuka  ndio wakati wanapata nafasi ya kuzugmza ubaya wako jambo hili linafaa kukoma

malkia wa bongo fleva, Zuchu
malkia wa bongo fleva, Zuchu
Image: INSTAGRAM

Malkia wa Bongofleva Zuhura Othman almaarufu Zuchu  amefunguka kwa kuchoshwa na tuhuma za watu kwenye mitandao wakimtaka aolewe.

Zuchu kupitia kwenye mahojiano ya moja kwa moja na wanablogu wa mitandao nchini Tanzania amesimulia tetesi nyingi anazozipata kwenye mitandao kuhusu uhusiano wake na bosi wake Diamond Platnumz.

"Mwenyezi Mungu ndio mwanzilishi wa Ndoa, na pia nafahamu ndoa ni kama kifo hutokea kwa maisha ya mwanadamu wakati asipofahamu kwa hivyo wafuasi wetu kwenye mitandao ya kijamii wawe na subira mwenyenzi Mungu ndio anajua maisha ya ndoa kwa kila mmoja",alisema.

Zuchu alikiri kwamba yuko vyema na mahusiano yake na mpenzi wake Diamond akitaja pia kushagazwa na uvumi kwenye mitandao kuhusu chuki yake na mama Dangote akitaja kuwa yeye na mamamkwe wako salama na wanazugumza kila wakati.

Msanii huyo kwenye mahojiano haya alisimulia kuwa wasanii wengi hupitia maneno mengi makali kwa mitandao ya kijamii ila kwake jambo hilo limekuwa la kawaida akisema kuwa mara nyingi tu wafuasi wao kwenye kurasa za mitandao huwarushia maneno yasiyo na msingi wowote,

"Wanamitandao wengi ukifanya jambo zuri kamwe wanaliacha ila wakati jambo baya inazuka  ndio wakati wanapata nafasi ya kuzungumza ubaya wako jambo hili linafaa kukoma kamwe kwani linachangia chuki kwa maisha ya wasanii,"alisema Zuchu.