Diamond hajamuoa Zuchu sijui mahusiano yao -Khadija Kopa asimulia

Mahusiano ya Zuchu na Diamond siyajui ila sijafamishwa kwa vyovyote vile

Muhtasari

•Msanii Zuchu na Diamond  uvumi umeenea kwenye mitandao ya kijamii  wawili  hawa wakitajwa  kuwa pamoja katika mahusiano jambo ambalo mamake Zuchu Kadhija Kopa amesema kutolifahamu

Diamond Platnumz, Khadija Kopa, Zuchu
Diamond Platnumz, Khadija Kopa, Zuchu
Image: HISANI

Khadija Omari Kopa mwimbaji wa muziki wa Taarab na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Tanzania ambaye pia ni mamake mzazi msanii maarufu wa Bongo Zuchu amezungumzia swala ya mahusiano ya ndoa kati ya Bintiye Zuchu na Msanii Diamond.

Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na wanablogu wa mitandao Khadija Kopa alisimulia kutojua mahusiano hayo kwa kuwa Bintiye Zuchu hajamfamisha  kwa vyovyote vile kuhusu mahusiano yake.

"Mahusiano ya Zuchu na Diamond siyajui ila sijafamishwa kwa  vyovyote vile kulingana na mila zetu mshichana anapopata mume lazima wazazi wajulishe kwa pande mbili zote ndiposa swala la kulipiwa mahari itekelezwe kwa wakati  unaofaa kwa hivo Diamond na binti yangu Zuchu hawajaona ",alisema Kadhija Kopa.

Msanii Zuchu na Diamond  uvumi  wa wabea umeenea  kwenye mitandao ya kijamii wasanii hawa  wakitajwa  kuwa pamoja katika mahusiano jambo ambalo mamake Zuchu Kadhija Kopa amewaambia wanablogu kwamba jambo hilo kwani ni geni kwani anafahamu mapenzi halali ni ya kulipiwa mahari.

Katika mahojiano hayo Mtunzi wa Taarab aliwataka wanablogu kupata maelezo ya mapenzi hayo kutako kwa Bintiye Zuchu kwani hajapata ripoti yoyote kutoka kwake.