Paula amlisha mpenziwe Marioo keki kwa kutumia midomo mbele ya mamake, Kajala (video)

“Bosi huyo bosi bosi huyo bosi bosi huyo bosi,” watu wlaishangilia huku Marioo akiuma keki kutoka kwa mdomo wa Paula.

Muhtasari

• Binti huyo wa muigizaji mkongwe Kajala Masanja aliwalisha keki mama yake lakini pia mpenzi wake Marioo kwa njia ya kipekee.

Marioo na Paula
Marioo na Paula
Image: Screengrab

Mapenzi ya Marioo kwa mrembo Paula Kajala Masanja yanazidi kukwea kwenda viwango vingine.

Wikendi iliyopita Paula alikuwa na hafla ya kuzindua duka lingine la nguo na alitenga muda wa kuwalisha watu wake wa karibu keki kama kusherehehea hatua nyingine katika maisha yake.

Binti huyo wa muigizaji mkongwe Kajala Masanja aliwalisha keki mama yake lakini pia mpenzi wake Marioo kwa njia ya kipekee.

Katika video ambayo inaenezwa kwenye mitandao ya kijamii, Paula baada ya kumlisha mamake keki, ilikuwa zamu ya kumlisha mpenzi wake na safari hii hakutumia kijiko wala mikono.

Kwa utaratibu, Paula alimega keke na kuiweka kwenye meno yake kabla ya kumlisha Marioo ambaye aliing’ata kwa ustadi huku midomo yao ikigusana na kuvutia vifijo na mbwembwe kutoka wa umati wa watu wa karibu waliohudhuria.

“Bosi huyo bosi bosi huyo bosi bosi huyo bosi,” watu wlaishangilia huku Marioo akiuma keki kutoka kwa mdomo wa Paula huku mamake akiwapigia makofi ya pongezi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Marioo alipakia picha ya Paula na bila kutoa maelezo Zaidi kuhusu tukio la kulishana keki, alimpa hongera tu na kudokeza kwamba kuna kitu kikubwa ambacho anasubiria kufanyika.

“Hongera mpenzi wangu ️ @therealpaulahkajala najivunia wewe 🙈 I can't wait 💕” Marioo alisema.

Hata hivyo, baadhi waling’aka wakikisia kwamba huenda ni mimba wanasubiria, lakini bado si Marioo, Kajala wala Paula mwenyewe ambao wamethibitisha.

Hatua hii inakuja takribani miezi miwili baada ya Paula katika kipindi cha maswali na waandishi wa habari za mitandaoni kudai kwamba Marioo tayari ameshatoa posa kwa mamake Kajala na hata kutoa mahari ya shilingi za kitanzania milioni 100.

“Tayari ametoa mahari milioni 100,” Paula alijibu swali hilo huku wakicheka na mama yake na kujaribu kuficha nyuso.