Rotimi atumia Kiswahili kumtania Wolper baada ya kufanya challenge ya ngoma yake

Rotimi aliweka emoji za kucheka na kusema kwamba kwa miaka michache wamekuwa na Vanessa Mdee, ameweza kujifunza maneno kadhaa katika lugha ya Kiswahili.

Muhtasari

• Rotimi alicheka na kukiri kwamba kwa miaka michache ambayo amekuwa na Vanessa Mdee nchini Marekani, amejifunza machache kuhusu Kiswahili.

• “lol I learned a couple things over the years, sis😂! Najifunza, Asante Sana,” Rotimi alijibu.

Rotimi.
Rotimi.
Image: Instagram

Shemeji wa Watanzania kutoka Marekani, Rotimi amewashushua watanzania baada ya kutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasaha wakati anampongeza mmoja wa mashemeji zake, mwigizaji Jackline Wolper.

Picha lilianza pale Wolper alipakia klipu fupi kwenye Instagram yake akiwa na wanawe wawili na kwa umbali alikuwa anasikiliza na kucheza wimbo wa Rotimi.

Wolper, ama ukipenda mama P alisema kwamba kwa hali ya anga ambayo ni kijibaridi katika sehemu nyingi, alilazimika kukaa tu ndani na wanawe kujivinjari.

Kwa hali ya hewa hii watoto wangu vipenz vyangu ndo maBestie zangu wa kunifariji” aliandika.

Hapo ndipo watu wengi walifika na kuachia komenti zao na mmoja kati ya hao ni Rotimi mwenyewe ambaye alionesha furaha kwa shemeji yake kuonesha kuukubali wimbo wake.

Alimwandikia;

“Umetishaaaa dada.”

Akimjibu, Wolper alimpongeza Rotimi kwa wimbo huo mkali, tena kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

“Sawa shem Nyimbo kali kinoma haya mpe Dada hapo akupe habari ya haya Maneo yani nyimbo yako Niyakufunga Mwaka🙌besteeeee.”

Rotimi alicheka na kukiri kwamba kwa miaka michache ambayo amekuwa na Vanessa Mdee nchini Marekani, amejifunza machache kuhusu Kiswahili.

“lol I learned a couple things over the years, sis😂! Najifunza, Asante Sana,” Rotimi alijibu.

Komenti hii ilivutia maoni kadha wa kadha, baadhi wakicheka kwa furaha kwa shemeji yao kung’amua Kiswahili lakini pia wapo wengine waliosema kwamba huyo atakuwa ni mkewe Vanessa Mdee aliyeingia kwenye akaunti yake na kuandika kwa chapisho la Wolper.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya Watanzania;

“Muandiko wa vanessa huu😂😂” Tzdee alisema.

“aaaah weeeeee huyu n mpare kaandika😂😂😂😂😂😂😂😂” Mushy Spora.

“Hee huu sio mwandiko wako,” mwingine alimwambia Rotimi.

Ikumbukwe Rotimi ni msanii na mwigizaji kutoka Marekani mwenye asili yake nchini Nigeria.