Nataka kuwaonesha jinsi ninavyowapenda Wakenya - Koffi kuhusu lengo la shoo yake (video)

“Kila mtu, vijana, kina mama na wanaume njoo nyote mjumuike name katika shoo ya moja kwa moja kati ya tarehe 8 na 9 Desemba, Nairobi." alisema.

Muhtasari

• Hii itakuwa mara yake ya kwanza kurudi Kenya kufuatia kisa cha utatanishi kilichomhusisha 2016 ambapo alionekana kwenye video alimburuza mrembo.

Koffi Olomide
Koffi Olomide
Image: Facebook

Lejendari wa miziki ya Rhumba kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Koffi Olomide amezidi kuongeza kuni kwenye shoo yake ya moto ambayo inatarajiwa kufanyika nchini Kenya mnamo Desemba 8 na 9.

Koffi ambaye anafanya ujio wake mkubwa tangu kisa kilichomsababisha kupigwa marufuku kutia guu lake kwenye ardhi ya Kenya miaka michache iliyopita alipakia klipu kwenye kurasa za mitandao ya kijamii akichagiza kwamba lengo lake kuu ni moja katika shoo hiyo – kuonesha ulimwengu jinsi anayowapenda Wakenya.

“Mopao anakuja Nairobi tarehe 8 na 9 Desemba. Itakuwa ni moto, nitakuwa narejea Kenya baada ya miaka mingi. Niliwamiss sana muda mrefu. Nataka kuwaonyesha kina cha mapenzi yangu kwenu,” Koffi alisema katika klipu hiyo.

Msanii huyo mkongwe katika tasnia ya muziki pendwa kwa vizazi vingi aliwasihi watu wa matabaka na jinsia zote kujitokeza kwa wingi katika shoo hiyo ili kujipakulia mapenzi yake pasi na kusubiri kuhadithiwa.

“Kila mtu, vijana, kina mama na wanaume njoo nyote mjumuike name katika shoo ya moja kwa moja kati ya tarehe 8 na 9 Desemba, Nairobi. Mopao anarejea Kenya, nawapenda,” alimaliza.

Ili kupata maelezo yote kuhusu tikiti, bonyeza linki zifuatazo;

Hii itakuwa mara yake ya kwanza kurudi Kenya kufuatia kisa cha utatanishi kilichomhusisha 2016 ambapo alionekana kwenye video alimburuza mrembo aliyetajwa kuwa mmoja wa wacheza densi wake.

Olomide akizungumza na Radio Jambo wiki jana kuhusu ujio wake unaosubiriwa kwa hamu na ghamu na wapenzi wa Rhumba, alishukuru uongozi wa Kenya na rais Ruto kwa kuhakikisha kwamba marufuku yake imetupiliwa mbali.

koffi olomide,
koffi olomide,

Pia alitaja mashabiki wake wa Kenya kuwa ni ‘ndugu zangu’ ambao amewamiss sana na itakuwa hafla kubwa ya kujumuika naoi li kuhakikisha kwamba analisafisha jina lake kwao.

Alisema kwamba kufutiliwa mbali kwa marufuku yake ya kukanyaga Kenya ni ishara kwamba haki imetendeka na kurejeshewa uhuru wake wa kutembelea Kenya.