Hata dunia ingeanza upya kesho bado ningetafuta nafasi ya kukuoa - Billnass kwa Nandy

“Napaswa Kumshukuru Mungu, Kwa Kunipa Mke na Rafiki ndani ya Nafsi Moja, Nakupenda sana Mke wangu" Billnass alisema.

Muhtasari

• "Nakupenda Mpaka Nakupenda tena ❤️ Happy Birthday 🎂 @officialnandy,” Billnass alimaliza.

Billnass na Nandy
Billnass na Nandy
Image: Instagram

Msanii Nandy Novemba 9, leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na mumewe Billnass amemtungia ujumbe maridhawa akimvisha koja la maua kwa kuwa mke na Zaidi mama mzuri wa kupigiwa mfano kwa maisha yake na mwanao, Kenaya.

Billnass alipakia picha ya siku yao ya harusi akimla denda Nandy na kusema kwamba hata siku moja ndani ya mwaka mmoja na miezi kadhaa ambayo wameishi pamoja kama mume na mke, hajawahi jutia uamuzi wa kumuoa malkia huyo wa Bongo Fleva.

Billnass alisema kwamba hata iwe kwamba dunia ilikuwa inafikia mwisho leo na kila kitu kurudishwa hatu ya kwanza, na yeye kesho aambiwe kufanya maamuzi upya ya kuchagua mrembo wa kuoa, basi bila shaka angemchagua Nandy tena na tena.

Napaswa Kumshukuru Mungu, Kwa Kunipa Mke na Rafiki ndani ya Nafsi Moja, Nakupenda sana Mke wangu…Hata Dunia ingeanza upya kesho bado ningetafuta Nafasi ya kukuoa!! Una kila sababu ya kunifanya Nikupende,” Billnass alimwandikia Nandy.

Msanii na mjasiriamali huyo wa bidhaa za kielektroniki pia alifichua kwamba furaha yake kwa asilia kubwa imetokana na uwepo wa Nandy katika maisha yake.

“Tabasam Langu na Furaha yangu ya Kila siku hutengenezwa na wewe… Heri ya Siku ya Kuzaliwa Mama @naya_bill Nina Mengi ya Kusimulia Ulimwengu Kuhusu upendo wangu kwako…ila Kwa leo wacha niseme Beki zangu Kwako Hazikabi kabisa…Nakupenda Mpaka Nakupenda tena ️ Happy Birthday 🎂 @officialnandy,” Billnass alimaliza.

Nandy kwa kujibu, alimuomba Mungu kuwalinda wote pamoja wala vishawishi visije kuingilia penzi lao.

“Aaaaaaaaaaaaaw 😵‍💫 nakupenda MUME WANGU sana sana sana sana MUNGU atutunze 😍 @billnass” Nandy alimjibu.

Wasanii hao wawili walifunga harusi mwaka jana wakiwa wanatarajia mwanao.

Hivi majuzi walisherehekea mwanao kufikisha mwaka mmoja na kutambulisha jina lake rasmi huku pia wikendi jana wakitoa taarifa njema kwamba tayari akiwa na mwaka mmoja ameshaanza kujiingizia mamilioni ya pesa kutokana na ubalozi wa mauzo kwa bidhaa za chapa mbalimbali.