Kwa mara ya kwanza Diamond Platnumz amerudia vazi alilolivaa mara ya mwisho 2019

“Nikuibie siri tu kwamba koti nililolivaa kwenye Komando ndilo koti lile lile nililolivaa zamani kwenye video ya Tetema." alisema.

Muhtasari

• Kupitia instastory yake, Diamond mwenyewe aliwafungua macho na wigo wa fikira mashabiki wake.

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: Screengrab//YouTube

Kwa mara ya kwanza tangu mwezi Februari mwaka 2019, msanii Diamond Platnumz amerudia nguo ambayo aliivaa mara ya mwisho mwaka huo kipindi wanafanya video ya Tetema – kolabo aliyoshirikishwa na Rayvanny.

Msanii huyo hivi majuzi ameachia kolabo ya Commando, akishirikishwa na msanii G Nako na katika moja ya scene, alionekana na koti rangi inakaribia kuwa waridi.

Mashabiki wengi hawakuweza kubaini kuwa koti hilo ndilo lile alilovaa wakati wanafanya video ya Tetema 2019.

Kupitia instastory yake, Diamond mwenyewe aliwafungua macho na wigo wa fikira mashabiki wake kwa kufichua kwamba ndilo lile lile vazi ambalo amelitunza kwa muda huo ambao unagonga Zaidi ya miaka minne na ushee.

Diamond alijipa hongera kwa utunzaji wa kipekee akisema kwamba si watu wengi ambao wanaweza onyesha mavazi yao ya miaka 4 iliyopita yakiwa katika hali shwari utadhani yametoka sokoni juzi.

“Nikuibie siri tu kwamba koti nililolivaa kwenye Komando ndilo koti lile lile nililolivaa zamani kwenye video ya Tetema. Hii inaitwa utunzaji na kuheshimu mali, kiufupi kutotumia hela ovyo,” Diamond alisema.

Ni adimu kwa wasanii na mastaa wengi kurudia nguo, Diamond akiwa mmoja wao ambaye huonekana na vazi moja kwa mara moja tu bila kulirudia.

Wewe hurudia nguo baada ya kipindi kipi?